Jane Mwakyoma ,Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro amewaomba wananchi na wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, kinachotarajiwa kufanyika mkoani humo
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Makongoro amesema kilele hicho kitafanyika Jumatano, Oktoba 14, 2026, katika viwanja vya Nelson Mandela, Manispaa ya Sumbawanga.
Amesema shughuli za kilele hicho zitaambatana na matukio mbalimbali, ikiwemo maonesho ya fursa na shughuli za vijana, yatakayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua kuanzia Oktoba 8 hadi Oktoba 14, 2026.
Aidha amesema kutakuwa na Misa ya Kumbukizi ya miaka 27 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itakayofanyika katika Kanisa Kuu Jimbo Katoliki Sumbawanga saa 12:00 asubuhi ya Oktoba 14, 2026, kabla ya kuendelea na sherehe za kilele cha Mwenge katika viwanja vya Nelson Mandela.
Aidha amewataka wananchi wa Rukwa kutumia fursa hiyo kujiinua kiuchumi kwa kufanya biashara mbalimbali, zikiwemo huduma za chakula, malazi, usafiri na usafirishaji kwa wageni watakaofika mkoani humo.
Amesema mkoa umejipanga kuhakikisha maandalizi ya kilele hicho yanafanyika kwa kushirikiana na Halmashauri zote nne,taasisi za umma, wadau na wananchi, huku akitoa wito kwa wananchi kushiriki katika kulinda amani na usalama wakati wa shughuli hizo .
Aidha Makongoro amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wananchi na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026 kinafanyika kwa mafanikio huku akiwataka wananchi kutumia tukio hilo kama fursa ya kukuza shughuli zao za kiuchumi na kudumisha amani na usalama wakati wote wa shughuli hizo.
Kilele hicho ni tukio muhimu la kihistoria kwa mkoa huo kuwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 24 kwa mkoa huo kuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ambapo uliwahi kuwashwa mkoani humo mwaka 1983 na 2002.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...