Na Janeth Raphael -MichuziTv -Bungeni Dodoma 


SERIKALI imeeleza mikakati mbalimbali inayotekelezwa katika kuendeleza michezo kwa watu wenye ulemavu, ikiwemo kuandaa makocha, kuendesha mashindano na matamasha ya michezo, pamoja na kuwawezesha wanamichezo wenye ulemavu kushiriki mashindano ya kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Nyamizi Simon Mhoja, aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuendeleza michezo kwa watu wenye ulemavu na kuzalisha wachezaji wenye ulemavu.

Waziri Makonda amesema Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa ya kushiriki na kuendeleza vipaji vyao katika michezo.

Amesema hatua hizo ni pamoja na kuandaa makocha wa michezo kwa watu wenye ulemavu, kuendesha matamasha yanayowashirikisha, kuandaa mashindano ya ndani ya michezo mbalimbali, pamoja na kuwezesha wanamichezo wenye ulemavu kushiriki mashindano ya kimataifa.

Aidha, Waziri Makonda amesema Serikali imeendelea kuhamasisha uanzishaji na usajili wa vyama vya michezo kwa watu wenye ulemavu, hatua inayolenga kuimarisha usimamizi na maendeleo ya michezo hiyo nchini.

Hadi Agosti 2026, jumla ya vyama tisa (9) vya michezo kwa watu wenye ulemavu vimesajiliwa, vikihusisha michezo mbalimbali ikiwemo soka, mpira wa kikapu, tenisi, riadha na kuogelea.

Hatua hizo zinaelezwa kuwa sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata mazingira bora ya kugundua, kukuza na kutumia vipaji vyao katika michezo, ndani na nje ya Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...