Profesa wa Sheria, Issa Shivji, amesema Watanzania hawawezi kukaa kimya wakati watoto na raia wa Palestina wakiendelea kuuawa katika Ukanda wa Gaza, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano wa Tanzania na Palestina pamoja na kusimamia haki ya wananchi wa Palestina.
Prof. Shivji ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika mkusanyiko wa kuonesha mshikamano na wananchi wa Palestina, hususan watoto wa Gaza wanaoendelea kukabiliwa na madhara ya vita na mashambulizi.
Amesema hakuna binadamu mwenye huruma anayeweza kubaki kimya anaposhuhudia mauaji na mateso dhidi ya watoto na raia, akisisitiza kuwa suala la Palestina si la Wapalestina pekee, bali ni suala linalopaswa kugusa dhamira ya wanadamu wote.
“Kama wewe ni binadamu, huwezi kukaa kimya wakati watoto wanauliwa, wakati watu wanauliwa na mauaji yanaendelea pale Gaza.”
Prof. Shivji pia amerejea historia ya Tanzania katika kupigania uhuru, kupinga ukoloni na ubaguzi, akisisitiza kuwa msimamo huo ulijengwa kwa kiasi kikubwa katika misingi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema Tanzania imekuwa na historia ya kuunga mkono harakati za ukombozi, ikiwemo harakati za Palestina, na imeendelea kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Palestina.
Kwa upande wake, Kassimu Hassan, mmoja wa viongozi wa Taasisi ya Friends of Palestine Tanzania, amesema mshikamano kati ya Tanzania na Palestina unapaswa kuendelea kuonyeshwa, hasa wakati watoto wa Palestina wanakabiliwa na mazingira magumu na kunyimwa haki ya kuishi na kucheza kwa amani kama watoto wa mataifa mengine.
Kassimu amesema jamii inapaswa kuendelea kupaza sauti katika kutetea haki, usalama na amani kwa watoto wa Palestina.
Pia amekumbusha msimamo wa kihistoria wa Tanzania katika kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina, akisisitiza umuhimu wa kizazi cha sasa kuendeleza mshikamano huo.
“Uhuru wa Palestina ni uhuru wetu sote. Viva Palestina, Freedom for Palestine,” amesema Kassimu Hassan.
Naye Mwanasheria na mwanachama wa Friends of Palestine Tanzania, Tina Mfanga, amesema Watanzania waliolelewa katika misingi ya kupigania uhuru iliyoasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere wataendelea kuunga mkono haki ya Palestina.
Tina amesema ni muhimu utamaduni huo ukarithiwe na kizazi kijacho, ndiyo maana watoto walihusishwa katika tukio hilo ili kuwafundisha historia ya mshikamano kati ya Tanzania na Palestina na kuwafanya wafahamu hali wanayopitia watoto wenzao wa Gaza.
Amesema watoto wanapaswa kufahamu madhila yanayowakabili wenzao wa Palestina, huku akisisitiza kuwa jamii haipaswi kukaa kimya mbele ya vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Tutaendeleza mapambano haya na tutaendelea kuwarithisha watoto wetu. Ndiyo maana kwenye tukio la leo tuko na watoto kama sehemu ya kuwarithisha utamaduni huu na kuwafundisha historia hii,” amesema Tina Mfanga.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...