Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, amesema CCM itaendelea kuboresha mazingira na huduma za kazi kwa watumishi wa Chama hicho, kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ndg. Abdi ameyasema hayo leo, Septemba 13, 2026, alipowasili katika Tawi la CCM Kivunge A, Jimbo la Kijini, ambapo amefurahishwa na hali ya uhai, umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama wa CCM katika jimbo hilo.

Amesema hali hiyo ni ishara ya mshikamano wa wanachama, jambo alilolitaja kuwa ni msingi muhimu katika kukiimarisha Chama na kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi, Ndg. Khamis Mbeto Khamis, amesema ziara hiyo inalenga kukagua na kutathmini hali ya uhai wa CCM kuanzia ngazi ya matawi hadi jimbo.

Aidha, amewataka wanachama wa CCM kuelekea uchaguzi wa ndani wa Chama mwaka 2027 kutumia fursa hiyo kuchagua viongozi bora, wenye uwezo wa kukiongoza Chama na kukivusha kwa mafanikio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Katika ziara hiyo, Ndg. Abdi pia amemtembelea na kumjulia hali Ndg. Khamis Ali Khamis nyumbani kwake Kivunge B, hatua aliyosema inalenga kuendelea kuonesha thamani ya kuwajali, kuwathamini na kuwakumbuka wazee pamoja na wanachama waliokitumikia Chama Cha Mapinduzi.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...