Vodacom Tanzania plc imeendelea kutumia mchezo wa golf kama jukwaa la kuunganisha viongozi wa biashara na makampuni, watoa maamuzi na wadau wa sekta mbalimbali, kupitia ushiriki na udhamini wake katika CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26 katika viwanja vya hotel Sea Cliff Golf Course, Zanzibar.
Mashindano hayo yamewakutanisha viongozi wa makampuni, maafisa watendaji wakuu (CEO’s), wanadiplomasia na wachezaji wa golf kutoka hapa nchini na mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Nigeria, huku yakishirikisha zaidi ya wachezaji 80 kutoka mataifa hayo.
Wachezaji wa golf kutoka Kenya, Thomas Mwangi na Caroline Muigai, wametwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume na wanawake mtawalia katika mashindano ya hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc.
Mwangi alitwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume baada ya kukusanya pointi 40, huku Muigai akiibuka kinara kwa wanawake kwa pointi 41 katika mashindano yaliyochezwa kwa mfumo wa Stableford kwenye mashimo 18.
Katika Division A, Patrick O’Rourke alitwaa nafasi ya kwanza, huku Ernest Sengeu akimaliza wa pili kwa pointi 31.
Thagaran Govender alishinda Division B kwa pointi 39, akifuatiwa na Gregory Eayrs aliyepata pointi 38. Katika Division C, Abbas Simkoko alitwaa ushindi kwa pointi 40, akifuatiwa na Joseph Sayi aliyepata pointi 37.
Kwa upande wa wanawake, Salome Gakere alishinda kwa pointi 36, huku Vicky Elias akimaliza nafasi ya pili baada ya kufungana pointi 35 na Maryanne Mugo na kuamua kwa mfumo wa countback.
Ushiriki wa Vodacom Tanzania katika mashindano hayo umeenda zaidi ya mchezo wa golf na kuwa sehemu ya namna kampuni inavyotumia majukwaa ya michezo kujenga mahusiano na jumuiya ya biashara, huku ikiunganisha teknolojia na huduma za kidijitali katika mahusiano hayo kwa lengo la kuchochea ukuaji wa biashara.
Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, alisema kampuni hiyo inajivunia kuunga mkono mashindano yanayounganisha michezo na jamii ya wafanyabiashara.
“Tunafurahi kudhamini na kushiriki mashindano ya CEO Golf Tournament kwa sababu gofu si mchezo pekee, bali ni jukwaa linalowakutanisha watu, mawazo na fursa,” alisema Kamando.
Alisema mashindano hayo yanatoa mazingira rafiki kwa viongozi wa biashara kutoka sekta mbalimbali kukutana na kujenga mahusiano ya kikazi.
Kamando pia alihusisha mashindano hayo na juhudi za kukuza utalii visiwani Zanzibar, akisema matukio ya kimataifa ya michezo yanaitangza Zanzibar kwa wageni ambao wanaweza kurejea kwa ajili ya utalii au shughuli za kibiashara.
“Tunajivunia kushiriki katika kuitangaza Zanzibar kama kituo cha biashara, utalii na michezo. Matukio kama haya yanaongeza thamani si kwa washiriki pekee, bali pia kwa uchumi kiujumla,”alisema.
Hivyo, ushiriki katika majukwaa kama CEO Golf Tournament unaipa Vodacom Tanzania nafasi ya kukutana na viongozi wanaofanya maamuzi katika sekta ya biashara, kusikiliza mahitaji yao na kuendeleza mazungumzo kuhusu namna teknolojia inavyoweza kusaidia biashara kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Kwa Vodacom Tanzania, ushiriki katika majukwaa ya golf unaendelea kuwa sehemu ya kujenga mahusiano na viongozi wa makampuni ya biashara, kubadilishana mawazo na kuendeleza fursa za ushirikiano katika dunia ya biashara inayozidi kuunganishwa na teknolojia.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (Kulia) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa jumla kwa upande wa wanaume Thomas Mwangi (kushoto) katika mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa tukio hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando akishiriki katika mashindano ya CEO Golf Tournament, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.
Mkuu wa idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business katika kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa divisheni A katika Mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, Ernest Sengeu (kushoto). Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.
Mkuu wa Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi (kulia) akikabidhiwa zawadi na afisa masoko wa kampuni hiyo Chelsea Njau, baada ya kuibuka mshindi wa Pili wa Mashindano ya CEO Golf Tournament 2026.
Mkuu wa Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business katika kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi akishiriki katika mashindano ya CEO Golf Tournament. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...