Na Janeth Raphael - MichuziTv
Wakala wa Vipimo (WMA) umesema jukumu la kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika biashara vinafanyika kwa usahihi, pamoja na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, lina msingi pia katika mafundisho yanayopatikana katika vitabu vya dini, ikiwemo Qur’an Tukufu na Biblia Takatifu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla, ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa mwaka 2025/26 pamoja na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2026/27.
Kihulla amesema maandiko matakatifu yanasisitiza umuhimu wa kufanya vipimo kwa usahihi, hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi na vilivyohakikiwa kwa mujibu wa sheria. Amesema hatua hiyo ni muhimu katika kujenga uadilifu na kuaminiana katika shughuli za biashara.
“Mtu anayetaka kufanya biashara afanye biashara iliyonyooka. Lazima awe na vipimo sahihi na ambavyo vimehakikiwa kwa mujibu wa sheria,” amesema Kihulla.
Amesema WMA, ikiwa ni sehemu ya safari ya kuelekea utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, itaendelea kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika shughuli mbalimbali vinaendana na viwango vinavyotakiwa. “Kilo moja ukipimiwa kweli iwe kilo moja, na si vinginevyo,” amesema.
Kwa mujibu wa Kihulla, usimamizi wa vipimo unalenga kujenga uaminifu katika biashara, kumlinda mlaji pamoja na mtoa huduma, huku ukiisaidia Serikali kupata mapato yanayostahili kupitia matumizi ya vipimo sahihi na vilivyohakikiwa.
Amesema WMA itaendelea kuwa chombo muhimu katika kuwezesha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, hususan katika kujenga mazingira ya biashara yenye uaminifu na hatimaye kuchangia ujenzi wa Taifa lenye uchumi imara, jumuishi na wenye ushindani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...