Na Janeth Raphael – MichuziTv
Wakala wa Vipimo (WMA) umewataka wafanyabiashara na wananchi kuacha kutumia madebe, makopo, mafungu na vifaa vingine visivyotambuliwa kisheria kama vipimo katika biashara, ukieleza kuwa matumizi ya vifaa hivyo ni kinyume cha sheria na yanaweza kuchukuliwa kuwa kosa la jinai.
Akizungumza leo jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa mwaka wa fedha 2025/26 na mwelekeo wa mwaka 2026/27, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla, amesema vipimo visivyo rasmi vinaweza kusababisha bidhaa kupimwa kwa viwango tofauti na hivyo kuwanyima haki watumiaji.
Kihulla amesema matumizi ya madebe na makopo katika kupima bidhaa kwa uzito hayatoi kipimo cha uhakika kwa kuwa kiasi kinachopatikana kinaweza kutofautiana kutoka chombo kimoja hadi kingine, jambo linaloweza kusababisha mfanyabiashara au mlaji kupata kiwango kisicho sahihi cha bidhaa anayolipia.
“Madebe, makopo, visado na mafungu sio vipimo na tumeendelea kutoa elimu kwa wananchi, lakini pia tunaendelea kuchukua hatua dhidi ya wanaojihusisha na upimaji wa aina hiyo,” amesema Kihulla.
Amesema WMA itaendelea kusimamia matumizi ya vipimo sahihi kwa lengo la kuhakikisha biashara zinafanyika kwa haki na kulinda maslahi ya wafanyabiashara pamoja na watumiaji, huku akiwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanakuwa na mizani inayokidhi matakwa ya kisheria katika maeneo yao ya biashara.
Aidha, Kihulla amewahimiza wananchi kujenga utamaduni wa kuhakikisha bidhaa wanazonunua zinapimwa kwa mizani sahihi, akisisitiza kuwa matumizi ya vipimo vinavyotambulika kisheria ni sehemu muhimu ya kulinda haki za mlaji na kuhakikisha kila mmoja anapata kiwango cha bidhaa anachostahili.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...