NA DENIS MLOWE IRINGA
JESHI la Polisi nchini, kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, limepokea vifaa maalumu vya kuongozea magari vilivyotolewa na mdau wa maendeleo kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani na kupunguza changamoto za foleni katika Mlima Kitonga, barabara kuu ya Iringa–Morogoro
Vifaa hivyo vimetolewa na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya WILNA INTERNATIONAL, Willy Ngoya, Mtanzania anayeishi nchini Japan, ambaye amesema ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na juhudi za askari wa Jeshi la Polisi katika kuwasaidia wananchi wanaokumbwa na changamoto ya foleni katika eneo hilo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, Ngoya alisema amevutiwa na utendaji kazi wa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, S/SGT Marcus Mongo, baada ya kuona taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari zikimuonesha akifanya kazi kwa bidii kuhakikisha magari yanapita na kupunguza kero inayowakabili watumiaji wa barabara katika Mlima Kitonga.
Alisema juhudi za askari huyo zimempa msukumo wa kuchangia vifaa hivyo ili kurahisisha majukumu ya askari, hasa katika eneo hilo ambalo linahitaji uangalizi wa karibu wa usalama barabarani na uratibu wa magari.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni taa za kuongozea magari wakati wa usiku, jaketi maalumu za kujikinga na joto, viakisi mwanga kwa matumizi ya usiku, kamera za kurekodi matukio pamoja na vifaa vingine vya kazi.
Ngoya alisema anaamini msaada huo utaboresha mazingira ya kazi kwa askari wa usalama barabarani na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi, hususan wakati wa kukabiliana na foleni na changamoto nyingine zinazoweza kujitokeza katika eneo la Mlima Kitonga.
Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inalenga kuimarisha uhusiano kati ya jamii na Jeshi la Polisi kwa kutambua na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na askari katika kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake, S/SGT Marcus Mongo aliishukuru Kampuni ya WILNA INTERNATIONAL kwa msaada huo, akisema vifaa hivyo vitasaidia kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na kuongeza ufanisi katika kukabiliana na changamoto za usalama barabarani.
Alisema vifaa hivyo ni muhimu katika kuimarisha uratibu wa magari na usalama wa askari wanapokuwa kazini, hasa nyakati za usiku na katika mazingira yenye changamoto za kiutendaji.
Msaada huo unaonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wa maendeleo na Jeshi la Polisi katika kuimarisha usalama barabarani na kuboresha huduma kwa wananchi wanaotumia barabara kuu ya Iringa–Mbeya.

.jpg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...