Na Victor Masangu,Kibaha


Uongozi wa Azania bank umesema kwamba utaendelea kushirikiana bega kwa bega na serikali ili kuweza kurudisha fadhila kwa jamii katika mambo mbali mbali ya kuleta chachu ya kimaendeleo katika sekta tofauti.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Azania bank tawi la Kibaha Anna Monyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka 2026 ambayo yamefanyikia katika ofisi zao zilizopo katika jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Katika sherehe hizo ambazo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,wateja wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka ambapo pia walipa fursa ya kufunguliwa akaunti zao na kukabidhiwa kadi za ATM.

Meneja huyo amebainisha kwamba lengo lao kubwa kama Azania bank ni kuendelea kuweka mipango madhubuti ya kuwahudumia wateja wao ikiwa pamoja na kurudisha fadhila kwa jamii na kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.

"Kipekee kabisa mimi meneja wa Azania bank tawi la Kibaha napenda kuchukua fursa hii ya kipekee kuwashukuru kwa dhati wateja wetu kwa kuweza kuendelea kutuamini na sisi tupo tayari kuwahudumia,"amebainisha Meneja huyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka ameipongeza kwa dhati Bank ya Azania kwa kuweza kuona umuhumu wa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wa Kibaha ambapo hapo awali walikuwa wakipata usumbufu katika kuifuata huduma hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mhe.Koka amebainisha kwamba uongozi wa Azania bank umekuwa mstari wa mbele kushirikiana bega kwa bega na serikali pamoja na wateja wao kwa lengo la kuweza kuleta chachu ya uchumi.

Naye Afisa mfawidhi wa PSSF Mkoa wa Pwani John Mwalisu ameupongeza uongozi wa Azania bank kwa kuweza kuweka mikakati ya kupanua wigo wa kufungua matawi katika maeneo mbali mbali ikiwemo Tawi la Kibaha.

Nao baadhi ya wateja wa Azania bank waliopata kushiriki katika tukio hilo la maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja wameridhishwa na huduma zinazotolewa na kufurahishwa na ujio wa ofisi za tawi hilo kuja Kibaha.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...