MISS Kinondoni wajinadi na Kujisifu kutoa Miss Tanzania  huku wakisisitiza kuwa misimu yote ya mashindano hayo Wilaya hiyo imekuwa ikifanya vizuri na ikiwa na upinzani mkubwa sana wa Kikanda na Mikoa mingine. 

 Muandaaji wa shindano hilo Salome Kikwembe amesema mwaka huu ni wa kipekee kwa kuwa wamepewa jukumu la kuwa waandaaji wa Miss Kinondoni 2026 kutoka kwa Mkurugenzi wa Lamata Village ambae ndio Muendeshaji wa Mashindano hayo ya ngazi ya Kitaifa pamoja na Kanda zote.Aidha Muandaaji huyo , ameeleza kuwa maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri kambini na warembo wapo tayari kushiriki katika mchakato wa kuwania taji hilo hadi ngazi ya Kitaifa  na kujisifu kuwa Miss Kinondoni 2026 inaenda kuweka historia iliyoachwa Misimu nane ya mashindano ya Miss Tanzania  akimtaja Miss Tanzania 1998 Basilla Mwanukuzi, Miss Tanzania 2004 Faraja Kotta,Miss Tanzania 2005 Nancy Sumari ,Miss Tanzania Wema sepetu 2006,Miss Tanzania 2007 Richa Adhia ,Miss Tanzania  2012 Brigitte Alfred,Miss Tanzania 2016 Diana flavian,Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth makune. 

Pia Kikwembe amesema tayari washiriki 15 wapo kambini na wanaendelea na mazoezi klabu Masai Mwananyamala Jijini Dar es Salaam tunategemea kuwa na mashindano madogo kabla ya kilele chake Oktoba 25,2026 katika Ukumbi wa Serena Hotel Jijini Dar es Salaam. 

Mbali na taji kuu, mashindano hayo pia yatakuwa na tuzo ndogondogo zitakazotolewa kwa washiriki katika vipengele mbalimbali, vikiwemo Miss Photogenic, Miss Talent, Top Model, Top Sports Woman na Miss Personality.

Aidha Kikwembe ameongeza kuwa Lengo la Shindano hilo ni kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa jukwaa la kukuza vipaji, kuhamasisha uwajibikaji wa kijamii na kutoa fursa kwa washiriki kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...