Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Pius Chatanda (MCC), amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kuwa imara na kusimamia utekelezaji wa Ilani yake kwa lengo la kushughulikia changamoto za wananchi na kuimarisha maendeleo.

Chatanda ameyasema hayo leo, Oktoba 23, 2026, wakati akiendelea na mikutano ya ndani katika Kata ya Ikowa, Kijiji cha Makoja, Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo hilo.

Amesema wananchi hawapaswi kuyumbishwa na kauli mbalimbali, bali wanapaswa kuzingatia mipango ya maendeleo inayotekelezwa kwa mujibu wa sera na Ilani ya CCM.

Ameeleza kuwa mgombea wa ubunge kupitia CCM, Dkt. Netho Ndilito, endapo atapata ridhaa ya wananchi, atakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho na kuwasilisha mahitaji ya wananchi wa Chamwino katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Chatanda amesema mbunge ana jukumu la kuwa kiunganishi kati ya wananchi na Serikali, hususan katika kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...