Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeshika nafasi ya pili kwa kupewa Tuzo Maalum kama Mshindi wa pili Mamlaka ya Serikali za Mitaa Maonesho ya 09 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2026.

Tuzo hizo zimetolewa Oktoba 02,2026 na Mgeni Rasmi Dkt. Latifa Mohammed Khamis, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro ametoa Shukrani kwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusimamia vema sekta ya madini katika kuendesha uchumi wa viwanda, kuimarisha biashara ya nje kwa kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani , na kutoa ajira kwa vijana wengi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Hii inatokana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025-2050 inavyotambua kwa kina umuhimu wa sekta ya madini ili kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi imara, jumuishi na shindani kimataifa.

Aidha Mkurugenzi amewashukuru washiriki wote katika Maonesho hayo vikiwepo vikundi mbalimbali ambavyo Halmashauri imeviwezesha kushiriki Maonesho hayo ya Teknolojia ya Madini.

Maenesho hayo yana Kauli mbiu isemayo, "Madini ni utajiri-Tuwajibike kwa pamoja kufikia Dira ya Taifa 2050".


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...