Na Denis Mlowe, Iringa
HALMASHAURI ya Wilaya ya Iringa imetenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji katika sekta za viwanda, kilimo na utalii, ikiwa ni mkakati wa kukuza uchumi, kuongeza ajira na kufungua fursa mpya za biashara kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Robert Masunya, alisema maeneo ya Ugwachanya na Pawaga yametengwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, yakiwemo mahindi na mpunga.
Alisema viwanda hivyo vitasaidia kuchakata mazao kabla ya kufikishwa sokoni, kuongeza thamani ya bidhaa na kuwapa wakulima pamoja na wafanyabiashara wadogo na wa kati fursa za kushiriki katika mnyororo wa thamani wa mazao.
Masunya aliongeza kuwa halmashauri hiyo pia ina maeneo yanayolenga uwekezaji katika kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari, hatua inayotarajiwa kuchochea shughuli za kiuchumi kuanzia kwa wakulima hadi kwa wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali.
Alisema miradi hiyo inaweza kuongeza mahitaji ya huduma za usafirishaji, malazi, chakula na biashara nyingine, hivyo kupanua fursa za wananchi kunufaika na uwekezaji.
Katika sekta ya utalii, Masunya alisema halmashauri inaendelea kuweka mazingira ya uwekezaji katika ujenzi wa hoteli, viwanja vya michezo na gofu ili kuongeza huduma zinazoweza kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Alitaja maeneo ya Tungamalenga na Kihanga kuwa miongoni mwa maeneo yenye fursa za kuendeleza miundombinu ya malazi na michezo, akieleza kuwa uwekezaji huo unaweza kuimarisha utalii kwa kuunganisha huduma za malazi, burudani na safari za kutembelea vivutio vya asili, ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Alisema uwepo wa hoteli za viwango tofauti, kuanzia nyumba za kulala wageni hadi hoteli za hadhi ya juu, pamoja na viwanja vya michezo, unaweza kuongeza uwezo wa Iringa kupokea watalii, wachezaji na washiriki wa matukio mbalimbali.
Kwa mujibu wa Masunya, maendeleo hayo yanaweza pia kuchochea ukuaji wa biashara zinazohusiana na utalii na sekta ya ukarimu.
Akizungumzia namna ya kupata fursa hizo, aliwataka wawekezaji wanaohitaji kuwekeza katika wilaya hiyo kufika moja kwa moja katika ofisi za halmashauri ili kupata maelekezo kuhusu maeneo yanayofaa kwa miradi yao na taratibu zinazopaswa kufuatwa.
Alisisitiza umuhimu wa wawekezaji kupata taarifa sahihi kutoka katika mamlaka husika badala ya kutegemea watu wasiohusika rasmi katika taratibu za uwekezaji.
Masunya alisema halmashauri iko tayari kutoa ushauri kuhusu upatikanaji wa ardhi, masharti ya uwekezaji na uwezekano wa kuingia ubia na wawekezaji kwa kuzingatia sheria na mikataba inayotambulika kisheria.
Alieleza kuwa ardhi ni miongoni mwa mahitaji muhimu katika utekelezaji wa miradi ya uwekezaji, hivyo halmashauri iko tayari kujadili njia mbalimbali za kuwezesha miradi, ikiwemo ubia na utoaji wa ardhi kwa masharti yanayokubalika kisheria.
Alisisitiza kuwa uwekezaji katika viwanda, kilimo, utalii na huduma nyingine ni muhimu katika kupanua shughuli za kiuchumi, kuongeza ajira na kuweka mazingira yatakayowezesha wananchi wa Iringa kunufaika na fursa zitakazotokana na miradi hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...