Na Victor Masangu, Bagamoyo
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Pwani kwa juhudi za kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuendeleza sekta ya viwanda, akisema hatua hizo zina mchango muhimu katika kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira.
Mwigulu ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bagamoyo, ambapo alitembelea baadhi ya miradi ya uwekezaji na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kongani ya Viwanda ya Hongwang Tanzania (HWTZ) SEZ Limited.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wananchi waliotoa maeneo yao kwa ajili ya uwekezaji wanalipwa fidia stahiki ili kumaliza malalamiko na migogoro ya ardhi, huku utekelezaji wa miradi ukiendelea katika mazingira ya amani na ushirikiano.
Alisema Serikali imeweka chanzo maalumu cha fedha kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi hao, hatua inayolenga kuharakisha malipo na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo bila migogoro inayoweza kujitokeza kutokana na kuchelewa kwa fidia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Haroon Nyongo, alisema mkoa huo unaendelea kuvutia wawekezaji kutokana na juhudi zinazofanywa kuboresha mazingira ya uwekezaji na kupanua shughuli za uzalishaji viwandani.
Alisema Mkoa wa Pwani una jumla ya viwanda 1,768, vikiwemo viwanda vikubwa 503, vya kati 248 na vidogo 1,017, pamoja na kongani 35 za viwanda.
Takwimu hizo zinaonesha nafasi ya sekta ya viwanda katika shughuli za kiuchumi za mkoa huo, huku uwekezaji unaoendelea ukitarajiwa kuongeza uzalishaji, kupanua fursa za biashara na kuimarisha upatikanaji wa ajira kwa wananchi.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...