KATIBU wa NEC ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Uchumi na Fedha, Ndugu Jamal Kassim Ali, amewataka viongozi na watendaji wa chama kuimarisha usimamizi wa fedha kwa kuzingatia taratibu na mifumo iliyowekwa.

Jamal ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa chama, ambapo amesema mafunzo kuhusu usimamizi wa fedha tayari yametolewa kwa makatibu wa mikoa na yataendelea hadi ngazi ya wilaya, kwa lengo la kuwawezesha watendaji kusimamia rasilimali za chama kwa ufanisi na uwajibikaji zaidi.

Amesema CCM imeweka mfumo madhubuti wa usimamizi wa fedha za chama na kwamba fedha zote za chama zinapaswa kutumika kwa kuzingatia mfumo huo.

Hata hivyo, amesema wamebaini baadhi ya mapungufu katika utekelezaji wa taratibu za matumizi ya fedha, ikiwamo kutofuatwa kikamilifu kwa taratibu zilizowekwa pamoja na wakati mwingine kuombwa kwa kiasi cha fedha kinachozidi uhalisia wa mahitaji husika.

Jamal amezitaka Kamati za Siasa za mikoa na wilaya kutekeleza wajibu wake kwa kujadili kwa kina masuala yanayohusu fedha za chama na kuhakikisha maamuzi yanayofanyika yanazingatia taratibu, uhalisia wa mahitaji na maslahi ya chama.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa viongozi na watendaji kuwa waangalifu katika matumizi ya rasilimali za CCM, akieleza kuwa kila fedha inayotumika inapaswa kuelekezwa kwenye shughuli halali za chama na kutumika kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...