FARIDA MANGUBE MOROGORO
Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake Katika kilimo na mazingira, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeanzisha Taasisi ya Mabadiliko ya Tabianchi na Bioanuai, itakayolenga kuimarisha utafiti, ubunifu na teknolojia za kutafuta suluhisho zitakazolinda rasilimali za asili na kuongeza tija na ustahimilivu wa kilimo nchini.
Akizungumza katika Mahafali ya 48 Mwenyekiti wa Baraza la SUA, Andrew W. Massawe, amesema taasisi hiyo ni sehemu ya hatua za Chuo kuongeza nguvu katika utafiti na ubunifu unaolenga kutatua changamoto za mazingira, mabadiliko ya tabianchi na upotevu wa bioanuai. Amesema maarifa yanayozalishwa kupitia tafiti yanapaswa kutumika katika kuboresha sera, mipango na mikakati ya maendeleo ya Taifa.
Amesema pamoja na hatua hiyo, SUA imeendelea kutekeleza miradi 116 ya utafiti katika maeneo mbalimbali nchini, inayolenga kuzalisha maarifa, teknolojia na ubunifu wa kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.

Chuo pia kimepata idhini ya Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) kuendesha programu ya kikanda ya Shahada ya Umahiri katika Uhandisi na Usimamizi wa Umwagiliaji, itakayodahili wanafunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Massawe, programu hiyo itaongeza wataalamu wenye ujuzi mahsusi katika sekta ya umwagiliaji, ambayo ni muhimu katika kuongeza uzalishaji na tija ya kilimo, hasa wakati uzalishaji unaendelea kukabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi. SUA pia inaendelea kuboresha mitaala yake ili kuendana na mahitaji ya sekta za uzalishaji, sayansi na teknolojia pamoja na soko la ajira.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael T. Chibunda, amesema Chuo hicho kimeendelea kuimarisha utafiti, ubunifu na mafunzo yanayolenga kujibu changamoto za Taifa, hususan katika sekta ya kilimo.

Amesema SUA inaendelea kutekeleza miradi 116 ya utafiti katika maeneo mbalimbali nchini, inayolenga kuzalisha maarifa, teknolojia na ubunifu, pamoja na kutoa suluhisho kwa changamoto za kijamii na kiuchumi.
Profesa Chibunda amesema miongoni mwa hatua zilizopigwa ni kupata idhini ya Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) kwa SUA kuendesha programu ya kikanda ya Shahada ya Umahiri ya Sayansi katika Uhandisi na Usimamizi wa Umwagiliaji.

Amesema programu hiyo, ambayo itadahili wanafunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki, itaiimarisha SUA kuwa kitovu cha kikanda cha kuzalisha wataalamu wa umwagiliaji, ambao ni muhimu katika kuongeza uzalishaji na tija ya kilimo, hasa katika kukabiliana na changamoto za utegemezi wa mvua.
Aidha, Profesa Chibunda amesema Chuo kinaendelea kutekeleza Mradi wa Mabadiliko ya Kiuchumi katika Elimu ya Juu (HEET) kwa lengo la kuboresha miundombinu na mazingira ya kujifunzia na kufundishia, huku zaidi ya watumishi 226 wakiendelea na mafunzo ya umahiri na uzamivu ndani na nje ya nchi.

Amesema hatua hizo zinaenda sambamba na kuanzishwa kwa programu mpya tano za masomo na kuanza kwa shughuli za Kampuni ya Uzalishaji Mapato na Huduma za Chuo, hatua zinazolenga kuongeza uwezo wa SUA katika kutoa elimu yenye tija, kujitegemea kifedha na kuchangia maendeleo ya Taifa.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...