Na Byera Deus, Bukoba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Kido, amezindua awamu ya pili ya mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, unaolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi, hususan kaya zenye uhitaji, makundi maalumu, vikundi vya ushirika na jamii kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kanali Kido alisema jumla ya kaya 38,217 zenye wakazi 84,934 zinatarajiwa kusajiliwa katika awamu hiyo ili ziweze kunufaika na huduma za matibabu kupitia mpango huo.
Alisema kaya maskini zinazotambuliwa rasmi zitasajiliwa na Serikali bila kuchangia fedha, hatua inayolenga kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Aidha, alisema kaya nyingine, vikundi na vyama vya ushirika vitachangia Shilingi 150,000 kwa mwaka, huku kifurushi husika kikitarajiwa kugharamia huduma za afya kwa watu sita.
Kanali Kido aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuhakikisha mifumo ya usajili na utambuzi wa wanufaika inafika hadi vijijini na mitaani ili wananchi wote wanaostahili wapate fursa ya kusajiliwa.
Alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa Serikali, watendaji wa maeneo husika na wadau wengine ni muhimu katika kutoa elimu na taarifa sahihi kuhusu mpango huo na namna wananchi wanavyoweza kunufaika nao.
Kwa upande wake, Meneja wa NHIF mkoani Kagera, Ismail Kangeta, alisema katika awamu ya kwanza ya usajili, jumla ya kaya 15,284 zenye wakazi 67,451 zilisajiliwa, sawa na asilimia 76 ya lengo la usajili lililowekwa.
Kangeta alisema NHIF iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kwa ufanisi na kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Aliongeza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa bima ya afya katika kupunguza mzigo wa gharama za matibabu wanapohitaji huduma za afya.
Kaulimbiu ya mpango huo ni: “Bima ya Afya kwa Wote kwa Uhakika wa Matibabu.”

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...