Tanzania imeng'ara katika umoja wa Mataifa Afrika kwa utashi wa Uongozi katika Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye kupitia serikali yake imetoa kipaumbele kwa sekta ya Maji na kutanga fedha za kutekeleza miradi pamoja na usimamizi thabiti katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya uhakika ya maji safi na salama na kupiga hatua za haraka maeneo ambayo yalikua na changamoto kubwa kufikiwa na maji wakati kazi ya kuendelea kusambaza maeneo yote ikiendelea kwa kasi.
Rai hiyo imetolewa na viongozi wa Afrika katika mkutano wa Maraisi, Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wa Maji jijini Luanda nchini Angola kwenye Mkutano wa Maji kama Kiungo cha Amani
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki mkutano Mkutano huu leo tarehe 22 Oktoba 2026 unaongozwa na Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akimwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na unamjumuisha Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb.), Waziri wa Maji na wataalam wengine. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kuimarisha Utawala wa Rasilimali Maji Inayovuka Mipaka barani Afrika kama Nyenzo ya Kuzuia na Kutatua Migogoro.”
Majadiliano yamehusisha diplomasia ya maji na usimamizi wa rasilimali za maji zinazovuka mipaka; ushiriki wa jamii, wanawake na vijana; athari za mabadiliko ya tabianchi, uhamaji na migogoro; pamoja na uwekezaji katika miundombinu ya maji na kujenga uwezo.
Pamoja na mambo mengine, Ujumbe wa Tanzania imetatumia jukwaa hili kueleza mafanikio yake katika sekta ya maji, mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda na usimamizi wa pamoja wa mabonde, mito na maziwa.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...