Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Richard Atufigwege Kasesela, amewahimiza wanawake wilayani humo kutumia hekima, ujuzi na fursa mbalimbali za kiuchumi kujikwamua kimaisha, akisisitiza kuwa mwanamke imara ni msingi wa familia imara na jamii yenye maendeleo.

Kasesela ameyasema hayo wakati akizungumza katika Kongamano la Wanawake la Wilaya ya Mvomero lililobeba kaulimbiu isemayo “Hekima ya Mwanamke ni Nguvu ya Jamii, Mwanamke Imara Jamii Imara,” ambapo amesisitiza umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya familia na taifa.

Amesema wanawake wana nafasi kubwa katika kilimo, biashara, ujasiriamali, malezi na uongozi, hivyo amewahimiza kuanzisha biashara kulingana na uwezo wao, kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa, pamoja na kutumia fursa za mikopo na programu za uwezeshaji zinazotolewa na Serikali na taasisi za fedha.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wanawake kuwekeza katika elimu, mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha na matumizi ya teknolojia ili kuongeza thamani ya bidhaa zao, kupanua masoko na kukuza kipato.

Katika hatua nyingine, Kasesela ameitaka jamii kushirikiana kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake, zikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na vikwazo vya upatikanaji wa mitaji na elimu, huku akiwahimiza wanaume kuwaunga mkono wanawake katika shughuli za maendeleo na kushiriki majukumu ya kifamilia.

Amesisitiza kuwa Serikali na wadau wa maendeleo wanapaswa kuendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha wanawake kupata elimu, huduma bora za afya, rasilimali za uzalishaji na fursa za kiuchumi, pamoja na kushiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi yanayohusu maendeleo ya jamii.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...