NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Bi. Siwema H Jumaa, amewahamasisha watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga kushiriki Mbio za Kitonga (Kitonga Marathon) zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 31, 2026, katika Kata ya Ilula, Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.
Akizungumza wakati wa kuhamasisha ushiriki wa watumishi hao, mara baada ya kufika Mafinga Bi. Siwema alisema mbio hizo ni fursa muhimu ya kutangaza vivutio vya utalii wa asili vilivyopo Kilolo, kuhamasisha uwekezaji na kuimarisha juhudi za uhifadhi wa mazingira katika eneo la Mlima Kitonga.
Alisema washiriki wa mbio hizo watakimbia umbali wa kilomita tano, 10 na 21, huku ada ya ushiriki kwa kila umbali ikiwa Shilingi 50,000. Aidha, washiriki wa mbio za majaribio (Trial Run) watakaokimbia kilomita 11 na kupata mandhari nzuri ya Mlima Kitonga watalipia ada ya Shilingi 70,000.
Bi. Siwema alisema Kitonga Marathon inalenga kuhamasisha uhifadhi wa mali asili za Mlima Kitonga, kutangaza fursa za uwekezaji katika Wilaya ya Kilolo na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira.
Aliongeza kuwa mbio hizo zitasaidia kukuza utalii wa asili na kujenga mahusiano mazuri ya kikazi baina ya watumishi wa taasisi mbalimbali, hususan katika Mkoa wa Iringa.
“Mbio za Kitonga zitasaidia kutangaza vivutio vya utalii wa asili na kukuza utalii katika Wilaya ya Kilolo. Pia zitasaidia kujenga mahusiano mazuri kwa watumishi wa Mkoa wa Iringa. Baada ya marathon kutakuwa na tafrija ya pamoja (after-party) itakayowawezesha washiriki kufurahi pamoja hadi saa sita usiku,” alisema Bi. Siwema.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Julius Mwalongo, alisema watumishi wa halmashauri hiyo watatumia fursa ya kushiriki mbio hizo kuimarisha mahusiano ya kikazi na kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Alisema ushiriki huo pia utatoa nafasi kwa watumishi kutoka halmashauri hizo mbili kukutana, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Bi. Sima Bingileki, alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kwa kutoa hamasa kwa watumishi kushiriki mbio hizo, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi za umma na kuitangaza Kilolo kupitia michezo.
Alisema ushiriki wa watumishi katika Kitonga Marathon unatarajiwa kuongeza uelewa kuhusu fursa za utalii na uwekezaji zilizopo Kilolo, huku ukiimarisha mshikamano na mahusiano ya kikazi miongoni mwa watumishi wa umma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...