Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amezishauri Klabu za Jogingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanza kutumia klabu hizo kuzungumza kuhusu namna ya kuimarisha uchumi wao na maisha yao sambamba na kutumia fursa zilizopo ikiwemo kuomba mikipo inayotolewa na Serikali.

Mpogolo ametoa ushauri huo leo Oktoba 11,2026 jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mbio za pole za kilometa sata zilizoandaliwa na Shirikisho la Joging Wilaya ya Ilala (IJA)na kushirikisha klabu mbalimbali kutoka Wilaya ya Ilala na mikoa mbalimbali nchini.

“Niungane na Mkurugenzi wetu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya kwamba pamoja na kufanya jogingi ni vizuri tukazungumza na maisha yetu na uchumi wenu. Kutembea kufanya mazoezi ni aina mojawapo lakini ni namna gani tunapambana na maisha yetu na uchumi wetu.

“Ukiangalia wetu mpendwa Rais DK.Samia Suluhu Hassan alizindua dira ya Maendeleo ya miaka 25 kwa maana ya dira 2050.Katika mkakati ule ule wa kuwasaidia vijana kuanzia kubadili mtaala wa masomo lakini kuwasaidia na kuwawezesha kiuchumi.
“Baada ya miaka 25 wanataka kipato cha kila Mtanzania kiwe ni zaidi ya dola 1000.Huwezi kupata dola 1000 kwa kila Mtanzania ikiwa vijana wa Jogingi mtawaacha peke yao wakiwa wahangaika,”amesema Mpogolo.

Ameongeza hivyo wanajogingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wanapokutana kwenye vikao vyao vya jogingi wazungumze pia kuhusu uchumi.”kuu wa Wilaya,Mkurugenzi na Katibu Tawala tupo na tumeletwa na Rais DK.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuwatumikia .

“Niwaombe kuanzia leo kila mnapokaa katika vikao vyenu hakikisheni mnajadili kuhusu maisha na uchumi wetu ,tumieni fursa hiyo kupata mkopo inayotolewa na Serikali na sisi viongozi tupo tutawasaidia.”

Kuhusu jogingi iliyofanyika leo iliyopewa jina City to City amesema kauli mbiu yao inasema Jogingi kwa amani na Afcon salama hivyo moja ya jukumu kama vijana ni kuhakikisha tunalinda amani.

“Moja ya fahari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na moja ya fahari ya Rais Samia ni uwepo wa amani .Hivyo tuhakikisheni amani yetu inaendelea kuwepo katika nchi yetu ,Mkoa wa Wetu na Wilaya yetu.

“Vijana tunawajibu wa kuilinda na kuitetea amani yetu na hata Rais DK.Samia Suluhu Hassan wakati anazindua dira 2050 alisema haiwezi kutekelezwa kama hakuna amani, hivyo amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...