Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amezindua rasmi Awamu ya Pili ya uandikishaji wa wananchi katika mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, huku Serikali ikilenga kusajili kaya 625,000.
Uzinduzi huo umefanyika leo, Oktoba 22, 2026, katika Uwanja wa Sabasaba mkoani Mtwara, ambapo Mchengerwa amewataka viongozi, watumishi wa umma, sekta binafsi na wananchi kushirikiana kuhakikisha huduma hiyo inawafikia Watanzania wote bila ubaguzi.
Amesema mafanikio ya mpango huo yanahitaji ushiriki wa kila Mtanzania, akisisitiza kuwa jukumu la kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya haliwezi kuachiwa Serikali pekee.
Mchengerwa amesema awamu hiyo inalenga pia kupanua wigo wa usajili kwa wananchi wasio na uwezo wa kuchangia gharama za bima, pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi, yakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara, madereva wa bodaboda, mama lishe na wafanyakazi wa kampuni binafsi.
Ameeleza kuwa wananchi wataweza kujiunga kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) au kampuni binafsi za bima zilizoidhinishwa na Serikali, huku Serikali ikiendelea kugharamia bima kwa wananchi wasio na uwezo, watakaotambuliwa kupitia mamlaka husika kwa kushirikisha jamii na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumzia utekelezaji wa Awamu ya Kwanza, Waziri huyo amesema kaya 198,709 kati ya kaya 276,004 za wananchi wasio na uwezo zilihakikiwa na kupewa kadi za bima, sawa na asilimia 72 ya lengo lililowekwa.
Amesema Mkoa wa Mtwara uliibuka kinara kitaifa katika kuwafikia walengwa wa mpango huo, huku Serikali ikiendelea na juhudi za kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata fursa ya kupata huduma za afya kupitia Bima ya Afya kwa Wote.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...