Mchengerwa ametangaza hatua hiyo leo, Oktoba 22, 2026, mkoani Mtwara, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa usajili wa Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Pili, akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa jamii katika kuhakikisha elimu kuhusu bima hiyo inawafikia wananchi.
Amesema mabalozi hao watatoka katika makundi mbalimbali, yakiwemo viongozi wa dini na kimila, walimu, wataalamu wa afya, wasanii, wanamichezo, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na viongozi wa wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, mabalozi watakuwa na jukumu la kuelimisha na kuhamasisha wananchi kujiunga na bima hiyo, kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya kufuatilia maendeleo ya usajili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi.
Ameeleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utaambatana na tathmini za kila mwezi, ambapo mabalozi watakutana na Wakuu wa Wilaya kujadili maendeleo ya uandikishaji, huku taarifa za utekelezaji zikiwasilishwa Wizara ya Afya kila robo mwaka.
Aidha, amewataka wananchi kulinda uendelevu wa Bima ya Afya kwa Wote kwa kuepuka udanganyifu, ikiwemo kutumia kadi za watu wengine, kutoa taarifa za uongo na kuwasilisha madai ya huduma za afya ambazo hazikutolewa.
Mchengerwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya kidijitali na usimamizi wa kisheria kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), ili kuhakikisha watoa huduma za bima wanatimiza wajibu wao, madai yanashughulikiwa kwa haki na wanufaika wanapata huduma wanazostahili.
Akizungumzia matokeo ya utekelezaji wa mpango huo, amesema Awamu ya Kwanza iliwezesha kusajili kaya 198,709 za wananchi wasio na uwezo,huku awamu ya pili ikilenga kusajiri kaya 625,000


.jpeg)

.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...