Na Mwandishi Wetu, TANGA
Wakati saa ya uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Simba ikianza kusogea, viongozi wa matawi ya klabu hiyo Mkoa wa Tanga wamefunguka na kutoa wito kwa wanachama kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali zilizotangazwa, wakisisitiza umuhimu wa kupata viongozi watakaosimamia maendeleo ya klabu hiyo kwa miaka minne ijayo.
Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga, Edgar Mdime, amesema wanachama wenye sifa na vigezo wanapaswa kutumia fursa hiyo kuchukua fomu, kuzijaza na kuzirejesha kwa wakati ili waweze kushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za uongozi.
Mdime amesema uongozi wa matawi mkoani humo umepokea taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club kuhusu kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari 3, 2027.
Amesema Mkutano Mkuu huo ambao hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne, ni sehemu muhimu ya mchakato wa kuamua mustakabali wa uongozi wa klabu, hivyo wanachama wanapaswa kuonyesha mwitikio kwa kujitokeza kushiriki katika mchakato huo.
Akisisitiza msimamo wa uongozi wa matawi mkoani Tanga, Mdime amesema wanahitaji kuona wanachama wengi wenye nia njema na Simba wakijitokeza kuwania nafasi hizo ili klabu ipate viongozi watakaoshirikiana katika kuleta maboresho na kuendeleza mafanikio yake.
Ameongeza kuwa uchaguzi huo ni fursa inayopatikana baada ya kipindi cha miaka minne, hivyo wanachama hawapaswi kuipuuza bali kuitumia kuchangia mustakabali wa klabu yao.
AIGUSA TFF, BMT NA SERIKALI
Katika hatua nyingine, Mdime amevitaka vyombo vinavyosimamia masuala ya michezo nchini, ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Serikali, kuhakikisha Mkutano Mkuu wa Simba unafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na Katiba ya klabu hiyo.
Amesema ni muhimu taratibu zote zinazohusu mkutano huo kufuatwa ili kuhakikisha mchakato mzima unakwenda kwa mujibu wa misingi inayotambuliwa na Katiba ya Simba.
BAVUMA AUNGANA NA MDIME
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga, Bavuma Jr, ameunga mkono wito huo kwa kuwataka wanachama wenye sifa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali zilizotangazwa na klabu hiyo.
Bavuma amesema Simba inahitaji viongozi watakaokuwa tayari kubeba majukumu ya kuiongoza klabu na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika kipindi chote cha uongozi wao.
Amesema kwa upande wao kama viongozi wa matawi, wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa kushirikiana na makao makuu ili kuhakikisha klabu inapata mafanikio na kusonga mbele.
Ameeleza kuwa ushirikiano kati ya viongozi wa matawi na uongozi wa makao makuu ni jambo muhimu katika kuimarisha klabu na kufanikisha malengo yake.
Kwa ujumla, viongozi hao wa matawi ya Simba Mkoa wa Tanga wameeleza kuwa wanatarajia kuona wanachama wakitumia fursa ya uchaguzi huo kushiriki katika kuunda uongozi wa klabu kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...