Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imesema itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hiyo ili kuvutia watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Vijijini, Afisa Uhifadhi Mkuu anayeshughulikia Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Kassim Nyaki, amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kufikisha taarifa kwa watu wengi kwa wakati mmoja.
Amesema mamlaka hiyo itaendelea kutumia fursa ya vyombo vya habari kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, sambamba na kuvitangaza katika masoko ya utalii ya kimataifa.
Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Ngorongoro, CO II Hillary Kimaro, amesema Ngorongoro ni kitovu cha maajabu mengi (Destination of Many Wonders), kutokana na kuwa na vivutio mbalimbali vinavyojumuisha wanyamapori, malikale na urithi wa utamaduni.
Ameeleza kuwa eneo hilo la Urithi wa Dunia linatoa fursa ya kipekee kwa watalii kujionea maajabu ya asili, ikiwemo kuzaliwa kwa ndama na uhamaji wa nyumbu katika eneo la Ndutu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), Neville Meena, amelipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kutangaza vivutio vya utalii nchini.
Amesema ushirikiano kati ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari ni muhimu katika kuongeza uelewa kuhusu utalii wa Tanzania na kuvutia maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...