Na Victor Masangu, Kibaha
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, ameahidi kuchangia mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya majengo katika Shule ya Awali na Msingi ya The Finest iliyopo Kata ya Mkuza, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.
Meya huyo ametoa ahadi hiyo wakati wa mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali wa shule hiyo, akieleza kuwa ameguswa na juhudi zinazofanywa na uongozi wa shule katika kuwekeza na kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Dkt. Mawazo amesema ameridhishwa na uwekezaji uliofanywa na shule hiyo na kumpongeza mkurugenzi wake kwa jitihada za kuhakikisha watoto wanapata elimu bora.
“Nimekuja katika mahafali haya na kujionea uwekezaji uliofanyika. Ninampongeza kwa dhati mkurugenzi wa shule hii kwa juhudi zake za kuwekeza kwa watoto, kwani elimu ni jambo la msingi sana katika maendeleo ya jamii,” amesema Dkt. Mawazo.
Aidha, amewapongeza wawekezaji wanaojitokeza kuwekeza katika sekta ya elimu, akibainisha kuwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali, ambapo uwekezaji ulitawaliwa zaidi na taasisi kubwa, sasa vijana pia wanashiriki katika kuendeleza sekta hiyo.
Amesisitiza kuwa elimu ni msingi wa maendeleo na kwamba jamii inapaswa kuwekeza katika elimu ya watoto ili kuwawezesha kuendelea na masomo hadi ngazi ya chuo kikuu.
“Elimu ni kila kitu, hivyo lazima tuwekeze katika elimu kwa kusomesha watoto wetu. Hakuna namna nyingine; ni lazima tuwekeze ili watoto wasome hadi chuo kikuu, kwa sababu elimu ina thamani kubwa,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shule ya The Finest, Abubakar Allawi, amesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazokabili shule hiyo ni miundombinu ya barabara na majengo.
Allawi amesema shule hiyo ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu bora kwa gharama nafuu, ili kuwawezesha watoto na vijana wa Kibaha kupata elimu inayokidhi mahitaji ya wakati huu.
Ameongeza kuwa uongozi wa shule utaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine katika kuwekeza na kuboresha sekta ya elimu, kuanzia ngazi ya awali na kuendelea.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...