Waandaaji wa mashindano ya urembo ya Miss Kinondoni 2026 wamejipanga kuhakikisha wilaya hiyo inatoa mshindi wa taji la Miss Tanzania mwaka huu, wakieleza kuwa imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano hayo ya kitaifa kwa misimu mbalimbali.
Muandaaji wa mashindano hayo, Salome Kikwembe, amesema mwaka huu ni wa kipekee kwao baada ya kupewa jukumu la kuandaa Miss Kinondoni 2026 na Mkurugenzi wa Lamata Village, ambaye ndiye mwendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi ya taifa na kanda.
Amesema maandalizi yanaendelea vizuri kambini, huku washiriki wakiendelea na mazoezi na maandalizi ya kuwania taji hilo, wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa.
Kikwembe amesema Miss Kinondoni ina historia ya kutoa washindi wa Miss Tanzania, akiwataja Basilla Mwanukuzi (1998), Faraja Kotta (2004), Nancy Sumari (2005), Wema Sepetu (2006), Richa Adhia (2007), Brigitte Alfred (2012), Diana Flavian (2016) na Queen Elizabeth Makune (2018).
Amesema wanatarajia kufanya vizuri zaidi mwaka huu na kuweka historia mpya kupitia mashindano ya Miss Kinondoni 2026.
Kwa mujibu wa Kikwembe, washiriki 15 tayari wameingia kambini na wanaendelea na mazoezi katika Klabu ya Masai, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa kutakuwa na mashindano madogo kabla ya fainali zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2026, katika Ukumbi wa Serena Hotel, jijini Dar es Salaam.
Mbali na taji kuu, mashindano hayo yatakuwa na tuzo mbalimbali za kutambua vipaji na uwezo wa washiriki, zikiwemo Miss Photogenic, Miss Talent, Top Model, Top Sports Woman na Miss Personality.
Kikwembe amesema lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji vya washiriki, kuhamasisha uwajibikaji wa kijamii na kuwapa fursa ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii.

Muandaaji wa Shindano la Miss Kinondoni 2026 Salome Kikwembe akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Shindano hilo akiwaita wadau wa sekta ya urembo kuunga mkono Shindano hilo ili kutimiza ndoto za Wasichana hao
Baadhi ya Warembo watakaoshindania Taji la Miss Kinondoni 2026 ambapo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu katika Ukumbi wa Serena Hotel Jijini Dar es Salaam

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...