WASANII Na Watayarishaji Wa Kazi za Filamu Wamekumbushwa kufata taratibu na sheria zilizowekwa na walezi wa kazi zao za Sanaa (BODI YA FILAMU)kwa kuhakikiwa na kuhakikisha zinapata vibali ili kazi hizo ziweze kuwapa manufaa na kulinda maadili ya Kitanzania.
Akizungumza hayo Afisa Maendeleo ya Filamu Mwandamizi Clarence Venance chelesi Wakati wa Kuzinduliwa rasmi kwa Tamthilia ya Rehani katika Ukumbi wa Sinema Mlimani City Jijini Dar es, amesema Kuna changamoto kubwa iliyopo kwa Wasanii na kazi zao kutoweza kupata vibali pamoja na Wasanii hao kutotambulika katika bodi ya filamu kwa maana ya kukosa usajili.
"Sisi Kama bodi tumekuwa na elimu mbalimbali ambazo tunaendesha kwa kuhakikisha wasanii wanajisajili na kutambulika kisheria ambapo ukijisajili kuna faida nyingi kupata fursa mbalimbali za kikazi pamoja na bodi kumtambua msanii huyo anaendesha kazi zake za Sanaa kisheria na taratibu zote bila kuvunja maadili sababu kazi hizo zina madaraja umri sahihi kwa walengwa wa kazi hizo ni upi?,je hakuna tamaduni ambazo zimewekwa katika kazi hizo? na mengineyo."
Aidha ametoa pongezi kwa Wadau mbalimbali wanaoendelea kutoa supoti kwa Watayarishaji wa kazi kwani vipaji vingi vipya vinazalishwa siku hadi siku kutokana na uwepo wa wadau wa kupokea kazi hizo huku akimtaja mdau kama Startimes Limited ambae kwa sasa ameipokea Tamthilia ya "Rehani " ambayo imeandaliwa na Mtayarishaji Abdul Juma.
Nae Meneja Masoko na Maudhui kutoka Startimes David Malisa ameongeza kuwa mashirikiano hayo yanalenga kukuza vipaji na kuifikisha mbali tasnia ya Filamu za Kibongo kutokana na Kisimbuzi hicho kuonekana Kimataifa hivyo Wasanii wategemee fursa nyingi nchi za kigeni.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...