Na George Maziku, Bukombe

MGODI wa dhahabu wa Msasa Gold Mine uliopo Kata ya Lunzewe Magharibi wilayani Bukombe, mkoni Geita umejiandaa kikamilifu kuzikabili mvua kubwa za El -Nino zinazotabiriwa kuanza kunyesha mwezi huu au mapema mwezi Novemba.

Kwa sasa mgodi huo unaaminika kuwa ndio mkubwa kuliko migodi mingjne yote ya wachimbaji wadogo katika kanda ya ziwa, umejiandaa kwa kujenga miundombinu imara ya mitaro kuzunguka eneo lote la mgodi pamoja na mabanda yatakayofunika eneo lote la uzalishaji wa madini ya Dhahabu.

Hayo yameelezwa na Meneja Mkuu wa mgodi huo Kessy Maira wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake hivi karibuni.

Maira alisema hayo mara baada ya kupokea maagizo ya serikali kupitia Tume ya Madini Tanzania juu ya kujiaandaa kujikinga na athari za mvua za El Nino, uongozi wa mgodi wake ulitenga bajeti maalum ya kujenga na kuimarisha miundombinu ya mitaro na mabanda ili kuzuia maji kutuama eneo la mgodi huo.

"Tunaendelea vizuri na maandalizi ya kujikinga na athari za mvua za El Nino kama serikali ilivyoagiza. Tumetenga fedha kwaajili ya kujenga mitaro mipya na kuimarisha ya zamani ili kuhakikisha hakuna maji yanayosimama eneo lote la mgodi", alifafanua Maira.

Aliongeza, "Pia tumejenga mabanda makubwa na imara zaidi kwenye eneo la maduara ya uzalishaji ili kuzuia maji kuingia maduarani na hivyo kuwahakikishia usalama wachimbaji na kuwezesha kazi ya uchimbaji kuendelea kipindi chote cha masika", alisisitiza meneja Maira.

Nae Mkaguzi Mkuu wa mgodi huo James Nkamba aliupongeza uongozi wa Msasa Gold Gold Mine kwa kutekeleza kikamilifu ushauri wa kiusalama uliotolewa na Idara ya Ukaguzi anayoiongoza, ikiwemo ujenzi wa mitaro mikubwa na ya kisasa, pamoja na mabanda makubwa na imara kuzunguka eneo lote la mgodi ili kuzuia maji kutuama mgodini.

"Idara yangu ndio iliyoandaa mpango mzima wa usalama wa mgodi huu. Tuliandaa michoro ya mitaro kuzunguka mgodi wetu na tukaushauri uongozi kuijenga kisasa ili iwe imara na kuweza kuhimili mvua kubwa za El Nino zinazotabiriwa", alibainisha Nkamba.

"Pia tulishauri kujengwa mabanda makubwa na imara eneo la uchimbaji lenye maduara yanayofanya kazi ili kuzuia maji kuingia maduarani, kuwezesha uzalishaji kuendelea wakati wa masika ambapo uongozi umetekeleza kikamilifu", alisisitiza Mkaguzi huyo mkuu.

Aliongeza, "Lakini vile vile tumefanyia ukarabati mkubwa maduara yetu yote ikiwemo kufunga vizuri matimba (magogo) ili kuimarisha kuta za maduara yote na hivyo kuhakikjsha usalama kwa wachimbaji na watu wote wanaofanya kazi eneo la uchimbaji".

"Kwahihiyo tunapenda kuwahakikishia usalama wachimbaji, wawekezaji na wadau wote wa mgodi wetu, kazi zitaendelea kama kawaida wakati wote wa masika", alisisitiza Nkamba.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...