TIMU ya Kata ya Olbalbal imetwaa ubingwa wa mashindano ya Rhino Cup baada ya kuifunga timu ya Kata ya Nainokanoka mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliochezwa leo, Oktoba 8, 2026, katika Uwanja wa Makao, Kata ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Mchezo huo wa fainali ulikuwa wa ushindani mkubwa, huku timu zote zikionyesha kiwango kizuri cha soka kabla ya Olbalbal kuibuka na ushindi na kutwaa taji hilo.
Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu, timu ya Kata ya Endulen iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kata ya Ngoile.
Mchezo huo pia ulivutia kwa namna ya kipekee, baada ya kutawaliwa na mbinu na ufundi wa soka huku wanyamapori mbalimbali, wakiwemo twiga, ngiri, pundamilia na nyati, wakionekana pembezoni mwa uwanja wakishuhudia mchezo huo.
Akikabidhi kombe la ushindi kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Meneja wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa SACC, Gloria Bideberi, aliipongeza timu ya Olbalbal kwa kutwaa ubingwa huo.
Bideberi alisema mashindano ya Rhino Cup yanalenga kuibua na kukuza vipaji vya michezo miongoni mwa jamii, kuhamasisha shughuli za uhifadhi pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na jamii zinazoishi ndani ya eneo hilo.
Katika zawadi za ubingwa, timu ya Olbalbal imekabidhiwa kombe, fedha taslimu pamoja na fursa ya safari ya kwenda Jijini Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga, utakaochezwa Oktoba 10, 2026.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...