Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema ziara zake nchini Qatar, Hispania na Armenia zimefungua fursa za ushirikiano katika uwekezaji, michezo na uhifadhi wa mazingira.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 18 Oktoba 2026, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, akirejea kutoka ziara hizo.

Amesema kampuni ya Alfardan ya Qatar imeonesha nia ya kuwekeza Zanzibar, huku makubaliano kati ya Real Madrid Foundation na Unicorn Zanzibar Sports Limited yakilenga kukuza vipaji vya soka kwa vijana na kuimarisha uwezo wa makocha wa ndani.

Aidha, amesema ushiriki wake nchini Armenia umefungua fursa za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika uhifadhi wa mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda rasilimali za bahari.

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kutekeleza masuala yaliyojadiliwa na makubaliano yaliyofikiwa ili kuhakikisha ushirikiano huo unaleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi na kuchangia maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.














Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...