Na Mwandishi Wetu, Mbeya
SIKU chache tangu Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, kutoa maelekezo ya kuharakisha ujenzi wa barabara jijini Mbeya, kazi hiyo imeanza kushika kasi huku maeneo yaliyokuwa na changamoto ya upitaji yakifunguliwa ili kurahisisha shughuli za wananchi.
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, alisema wameendelea kufungua njia zinazotumiwa na wananchi ili kupunguza adha iliyokuwepo kutokana na ujenzi wa barabara hiyo.
Alisema eneo la Kabwe ni miongoni mwa maeneo yanayotekelezwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Sadaka kuelekea Physical 29, ambapo hatua mbalimbali zimechukuliwa kuhakikisha wananchi wanapata njia za kupita wakati ujenzi ukiendelea.
“Tumetambua jumla ya maeneo 116 kuanzia Msagala hadi Fisi ambayo yalihitaji kufunguliwa ili wananchi waweze kupita. Maeneo hayo tumeshayafungua na sasa tunaendelea kuyaboresha ili yaweze kupitika bila shida,” alisema Bishanga.
Aliongeza mkandarasi ameagizwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa kasi na kwa ubora unaotakiwa, huku hatua za kuweka saruji zikiendelea katika maeneo husika. Alisisitiza kuwa lengo ni kukamilisha mradi bila kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na wafanyabiashara.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Patrick Mwalunenge alisema ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo baada ya kutembelea maeneo ya mradi na kujionea kazi zinazoendelea chini ya usimamizi wa TANROADS na mkandarasi.
Alisema kasi hiyo imeongezeka na njia zinazopitiwa na wafanyabiashara na wasafirishaji zimeanza kufunguliwa, akitolea mfano eneo la Mdope ambako vifusi vimewekwa ili kurahisisha magari kuingia na kutoka katika maeneo ya biashara.
Alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutakuwa na manufaa makubwa kwa uchumi wa Mbeya Mjini, ikiwamo kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, kuongeza shughuli za biashara na kuboresha mwonekano wa jiji.
Aliwataka wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, akisema ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya jitihada za kuboresha miundombinu.
Pia aliwashauri wasimamizi wa mradi kuhakikisha maeneo ya biashara yanaendelea kufikika wakati ujenzi ukiendelea na kwamba sehemu ambazo bado hazijawekewa lami zimwagiwe maji ili kupunguza vumbi linaloweza kuathiri wafanyabiashara na wananchi wanaotumia barabara hizo.
Akizungumzia hali ilivyokuwa kabla ya kutolewa kwa maelekezo ya Makamu wa Rais, mmoja wa wananchi wa Jiji la Mbeya Amos John alisema kulikuwa na changamoto ya kupita katika baadhi ya njia za mitaa, hali iliyosababisha bajaji, bodaboda na magari kupata shida kufika katika maeneo mbalimbali.
Alisema baada ya maelekezo hayo, njia zimeanza kufunguliwa na kuwekwa vifusi, hatua ambayo imerahisisha usafirishaji na kupunguza usumbufu kwa wananchi wanaotumia barabara hizo.
Naye mwananchi mwingine anayefanya shughuli zake katika eneo la Mdope, karibu na vibao vya Shule ya Rwanda Nzovwe Emanuel Mwakalinga
alisema ameshuhudia maendeleo ya ujenzi huo kwa kasi kubwa, akieleza kuwa kuwekwa kwa vifusi kumeboresha upitaji wa magari na kurahisisha upatikanaji wa maeneo ya biashara.
Alisema pia hatua zilizochukuliwa katika kufungua njia za kuunganisha mitaa na barabara kuu zimeanza kusaidia wananchi waliokuwa wakipata shida kufika katika maeneo yao ya shughuli za kiuchumi.
Wananchi hao waliishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza mradi huo na kupongeza maelekezo ya Makamu wa Rais, wakisema wanatarajia barabara hiyo itakapokamilika itarahisisha usafiri, kuchochea biashara na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi jijini Mbeya.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)Mkoa Mbeya Mhandisi Suleiman Bishanga akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais Dk.Deogratius Ndejembi kuhusu ujenzi wa barabara jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa
Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Patrick Mwalunenge akizungumzia kasi ya ujenzi wa barabara katika Jiji la Mbeya ikiwa ni siku chache baada ya Makamu wa Rais Dk.Deogratius Ndejembi kutoka maelekezo kwa TANROADS Mkoa wa Mbeya kuharakisha ujenzi wa barabara.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...