Shirika la INADES Formation Tanzania limewataka wadau na jamii kuimarisha juhudi za kulinda punda kutokana na umuhimu wao katika shughuli za kiuchumi na kijamii, hususan kwa jamii zinazowategemea katika shughuli za kila siku.
Akizungumza Oktoba 21, 2026, jijini Dodoma, wakati wa mkutano wa mwaka wa Shirika la Mtandao wa Mashirika ya Ustawi wa Punda Tanzania (TADWO), Michael Kihwele, Mkuu wa Idara ya Mafunzo, kutoka INADES Formation Tanzania amesema ni muhimu wadau kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika kutafuta rasilimali fedha na kuimarisha mahusiano ili kuboresha ustawi wa punda nchini.
Amesema INADES Formation Tanzania, ambayo ni sehemu ya mtandao wa mashirika Barani Afrika yanayolenga kusaidia jamii kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii, imeshiriki katika mkutano huo kuwezesha ubadilishanaji wa uzoefu kuhusu utafutaji wa rasilimali fedha na ushirikiano baina ya wadau.
Kihwele amesisitiza kuwa punda wana mchango mkubwa katika maisha ya jamii, hivyo mkutano huo ni fursa ya kuimarisha juhudi za pamoja za kuwalinda dhidi ya hatari ya kupungua na kupotea, ili waendelee kunufaisha jamii zinazowategemea.


.jpeg)


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...