Na Victor Masangu, Pwani
UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani umeadhimisha Wiki ya Wanawake kwa kufanya matendo ya huruma kwa akina mama katika Kituo cha Afya Mkoani, kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, huku ukifanya usafi wa mazingira katika baadhi ya maeneo.
Maadhimisho hayo yameongozwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani, Zainabu Vullu, ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo kutoka ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata.
Katika kuadhimisha wiki hiyo, viongozi hao walitembelea Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Mkoani na kutoa mahitaji mbalimbali ya msingi kwa wanawake wajawazito na waliojifungua, ikiwemo sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kupaka, maji, juisi pamoja na mahitaji mengine.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Vullu alisema amefarijika kuungana na wanawake wenzake katika kuadhimisha wiki hiyo kwa kufanya matendo yenye kugusa maisha ya jamii.
“Kwa kweli nimefarijika sana kuungana na wanawake wenzetu katika siku hii muhimu ya wiki yetu. Tumeamua kufanya maadhimisho haya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kwa kufanya matendo ya huruma katika Kituo cha Afya Mkoani pamoja na usafi katika nyumba za Katibu wa UWT Mkoa na Katibu wa UWT Wilaya,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani, Aziza Omary, aliwataka wanawake kuwa na upendo na mshikamano, huku akiwahimiza kushirikiana katika shughuli mbalimbali za jumuiya na kuachana na makundi.
Alisema baada ya kukamilika kwa chaguzi mbalimbali, ni wakati wa wanawake kuunganisha nguvu na kushirikiana katika kuimarisha jumuiya hiyo.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini, Elina Mgonja, alisema maadhimisho hayo yamewapa fursa ya kufanya shughuli za kijamii, ikiwemo usafi na matendo ya huruma.
Aliwahimiza wanawake kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuijenga jumuiya hiyo kuanzia ngazi za chini, huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuchangia maendeleo ya jamii.
Awali, akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maadhimisho hayo, Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini, Cesilia Ndaru, alisema jumuiya hiyo imefanya shughuli mbalimbali za kijamii kuanzia ngazi za matawi na mashina.
Alisema pia wamewahimiza wanawake kuweka mikakati endelevu ya kuongeza wanachama wapya kwa lengo la kuimarisha jumuiya pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa upande wake, Katibu wa Kituo cha Afya Mkoani, Saimon Swai, aliwashukuru viongozi wa UWT Mkoa na Wilaya ya Kibaha Mjini kwa kuchagua kutumia maadhimisho hayo kutoa msaada kwa wanawake waliopo katika Wodi ya Wazazi.
Swai alisema msaada huo utasaidia kukidhi baadhi ya mahitaji ya akina mama pamoja na watoto wanaopatiwa huduma katika kituo hicho.
Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa kufanya matendo ya huruma katika Kituo cha Afya Mkoani pamoja na zoezi la usafi katika nyumba za Katibu wa UWT Mkoa na Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...