Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Kher James amewahimiza wananchi kuwa na desturi ya kuchangia damu ili kuokoa uhai wa wahanga ambao wanahitaji damu.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo leo October 24 Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kitengo cha damu salama wakati alipokuwa Mgeni wa Heshima katika hafla ya uchangiaji damu iliyoandaliwa na Rotary Iringa Club kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa.

Mh.Kheri amesema damu ni muhimu sana hasa kwa kina mama waliojifungua,waliopata ajali pamoja ma wagonjwa mbalimbali na lazima itoke kwa binadamu na si mahali pengine,hivyo ni wajibu wa wananchi kuchangia damu ili kuendelea kuokoa maisha ya wahitaji.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...