Mafunzo ya biashara, usafirishaji wa bidhaa na malipo salama yalenga kuwasaidia wajasiriamali wanawake kupanua masoko yao nje ya nchi.
Mwanza, Tanzania – Wanawake wajasiriamali 150 kutoka Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamepatiwa mafunzo ya namna ya kupanua biashara zao na kufikia masoko ya kimataifa kupitia teknolojia na ujuzi wa biashara, katika juhudi za kuongeza fursa zao za kiuchumi na ushindani wa bidhaa zinazozalishwa nchini.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Apps and Girls, yamelenga kuwajengea washiriki uwezo wa kutafuta wateja nje ya nchi, kuelewa taratibu za kusafirisha bidhaa na kutumia njia salama za kupokea malipo kutoka kwa wanunuzi wa kimataifa.
Hatua hiyo inalenga kuwasaidia wanawake wajasiriamali kuona fursa za kibiashara zaidi ya masoko wanayoyafikia kwa sasa, huku wakijengewa uelewa wa vitendo unaoweza kuwasaidia kujiandaa kuingia katika biashara ya kimataifa.
Akizungumza wakati wa warsha hiyo, Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Yas Tanzania, Rukia Mtingwa, amesema kampuni hiyo inaamini kuwa kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia maarifa na ujuzi sahihi ni hatua muhimu katika kukuza biashara zao na kuwafungulia milango ya fursa mpya za kiuchumi.
“Lengo letu ni kumuinua mwanamke mjasiriamali kiuchumi kwa kumpatia maarifa na ujuzi utakaomwezesha kukuza biashara yake na kuvuka mipaka ya eneo alilopo. Tunataka wanawake waone kuwa bidhaa zao zinaweza kupata wateja katika masoko ya nje ya nchi, ikiwa watajipanga vizuri na kutumia fursa zinazopatikana kupitia teknolojia,” amesema Mtingwa.
Amesema Mwanza ni mkoa wa pili kufikiwa na mafunzo hayo baada ya Dar es Salaam, huku Yas Tanzania ikijipanga kufika katika mikoa mingine kwa awamu ili kuwafikia wanawake wengi zaidi wenye nia ya kukuza biashara zao.
Kwa upande wake, Mwanzilishi Mwenza wa Apps and Girls, Maria Nyangi, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wanawake uwezo wa kuendesha biashara kwa kujiamini zaidi, kuelewa mahitaji ya wateja na kutumia mbinu zinazoweza kuongeza uwezekano wa bidhaa zao kupata soko.
Amesema pamoja na kuwa na bidhaa bora, wajasiriamali wanahitaji kujua namna ya kuziwasilisha kwa wateja, kuwashawishi kufanya manunuzi na kujenga uhusiano wa kibiashara unaoweza kusaidia biashara zao kukua kwa muda mrefu.
Katika kuimarisha uelewa wa washiriki kuhusu fursa za biashara na mahitaji ya kisheria, Afisa Masoko wa Bodi ya Nyama Tanzania, Kanda ya Ziwa, Patrick Muro, amewahimiza wanawake kuchangamkia fursa zilizopo katika tasnia ya nyama, akieleza umuhimu wa kutambua fursa zinazoweza kuwasaidia kupanua shughuli zao za kiuchumi.
Naye Dotto Emmanuel kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko amesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kujisajili kwa mujibu wa sheria na kuzingatia taratibu zinazohusika na biashara zao, hatua inayoweza kuwasaidia kufanya shughuli zao katika misingi rasmi na kujiandaa kwa fursa pana zaidi za kibiashara.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wameishukuru Yas Tanzania kwa kudhamini mafunzo hayo, wakisema yamewaongezea maarifa na hamasa ya kutimiza ndoto zao za kuuza bidhaa katika masoko ya nje ya nchi.
Wamesema elimu waliyoipata imewawezesha kutambua kuwa kupanua biashara hakutegemei tu kuwa na bidhaa, bali pia kuelewa mahitaji ya soko, kupata wateja, kufahamu taratibu za usafirishaji na kuhakikisha malipo yanafanyika kwa usalama.
Kupitia ushirikiano huo, Yas Tanzania na Apps and Girls zinaendelea kuweka msisitizo katika kuwawezesha wanawake kwa maarifa yanayoweza kuwasaidia kutumia fursa za teknolojia na biashara, kukuza shughuli zao na kuongeza ushiriki wao katika uchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...