Mkuu wa mkoa wa Iringa Komred Kheri James amewahakikishia Wananawake waishio Vijijini dhamira ya Serikali kuendelea kusogeza na kuimarisha miundombinu na utoaji wa huduma ili kuchochea ustawi na maendeleo ya jamii katika maeneo hayo.
Komred Kheri James amtoa maelezo hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anaishi kijijini,yaliofanyika kimkoa wilayani Kilolo katika kijiji cha Vitono Kata ya Uhambingeto.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Komred Kheri James ameeleza kuwa katika kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kumuinua Mwanamke wa kijijini kiuchumi na kijamii,Serikali imeongeza kasi ya kupeleka umeme katika vitongoji,usambazaji wa umeme,ujenzi wa shule karibu na maeneo ya wananchi,upatikanaji wa pembejeo,utoaji wa mikopo na ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuchochea shughuli za uzalishaji na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewapongeza Wanawake wote waishio Vijijini na kuwahimiza kutumia fursa zilizopo kujiimarisha na kukua kiuchumi na kijamii,na kawakumbusha kuwa Serikali itaendelea kutunga sera,sheria na kuweka mipango madhubuti ya kuwajengea uwezo na kuwainua wanawake wa Vijijini.
#Iringa Imara,Tutaijenga kwa Umoja na Uwajibikaji



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...