Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekataza wananchi kuchangishwa fedha za kununua mafuta ya magari ya kubebea wagonjwa (ambulance) yanayowapeleka wagonjwa katika hospitali za rufaa, akisisitiza kuwa mamlaka zinazoyasimamia zinapaswa kuhakikisha yana mafuta ya kutosha ili kutoa huduma kwa wakati.
Aidha, amesisitiza utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutokuzuia miili ya marehemu hospitalini kwa sababu ya madai ya malipo.
Mwigulu alitoa maelekezo hayo Oktoba 16, 2026, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu changamoto ya kuchangishwa fedha za mafuta ya magari ya wagonjwa katika hospitali ya wilaya hiyo.
Alisisitiza kuwa huduma za afya zinapaswa kutolewa kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi, huku mamlaka husika zikihakikisha magari ya wagonjwa yanakuwa tayari wakati wote kuwahudumia wanaohitaji rufaa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alivielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia ununuzi, usambazaji na matumizi ya dawa za Serikali ili kuhakikisha zinawafikia wananchi waliokusudiwa.
Alisema usimamizi wa dawa hizo ni muhimu katika kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na rasilimali za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumzia maendeleo ya uchumi, Mwigulu alisema sekta binafsi imara pamoja na uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mazao ni muhimu katika kuongeza ajira na kipato kwa wananchi.
Aliwahimiza wananchi kuchangamkia fursa za uwekezaji na uzalishaji mali, huku akisisitiza umuhimu wa matumizi bora ya ardhi na kufuata sheria na taratibu zinazotawala shughuli za uwekezaji.
Alieleza kuwa uwekezaji unaozingatia sheria na kutumia fursa zilizopo unaweza kuchochea shughuli za kiuchumi na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...