Mtaalamu wa masuala ya jinsia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Jane Msagati, amesema maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Mkulima Duniani ni fursa ya kutambua na kuthamini mchango wake katika uzalishaji wa chakula, kuanzia kilimo cha mazao na mbogamboga hadi ufugaji, ambao ni muhimu katika kuhakikisha familia na jamii zinapata chakula cha kutosha na lishe bora.
Amesema pamoja na mchango mkubwa wanaoutoa, wanawake wakulima bado wanakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa rasilimali, umiliki wa ardhi na mitaji kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na kiuchumi. Hata hivyo, amesema changamoto hizo hazijawazuia kuendelea kushiriki katika uzalishaji wa chakula, hivyo kuna umuhimu wa jamii kutambua juhudi zao na kuimarisha mifumo ya kuwaunga mkono.
Msagati amesema kupitia maadhimisho hayo yanayofanyika mkoani Tanga, FAO kwa kushirikiana na Mkoa wa Tanga na Wizara ya Kilimo inalenga kutambua na kupongeza wanawake wakulima kwa mchango wao, huku akihimiza jamii kushiriki katika kuwapa moyo na kuendeleza juhudi zao. Maadhimisho hayo pia ni fursa ya kuwakutanisha wanawake wakulima na wadau wengine katika kusherehekea mchango wao katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake wakulima ili kuongeza tija katika kilimo na kuimarisha usalama wa chakula nchini, amesema kutambua wanawake wakulima wanaofanya vizuri ni njia ya kuthamini juhudi na ubunifu wao, pamoja na kuhamasisha wengine kuona kilimo kama fursa ya kiuchumi.
Amesema ni muhimu kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo ili kuwawezesha wanawake kuongeza thamani ya mazao yao na kufikia masoko mapana zaidi, ameeleza kuwa uwezeshaji huo ni muhimu katika kuboresha lishe, kuongeza kipato cha familia na kuchochea maendeleo ya taifa kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Peter Msofe, amesema Wizara ya Kilimo inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya sekta ya kilimo na kuhakikisha nchi inakuwa na chakula cha kutosha. Amesema wanawake ni sehemu muhimu ya mafanikio ya uzalishaji wa chakula kupitia hatua mbalimbali, kuanzia kulima, kupanda na kuvuna mazao hadi kuandaa chakula majumbani, hivyo juhudi zao zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa katika kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Tanzania, Charles Tulahi, amesema kuwawezesha wanawake na vijana kwa kuwapatia teknolojia, rasilimali na fursa za masoko ni muhimu katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kuboresha lishe na kuimarisha ustawi wa familia.
Amesema kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, wanawake wakulima wanapaswa kuwa sehemu muhimu ya maamuzi na mabadiliko katika mifumo ya chakula, ameeleza kuwa uwekezaji kwa wanawake na vijana utasaidia kujenga mifumo ya chakula jumuishi na endelevu, inayohakikisha wananchi wanapata chakula salama na chenye lishe bora.
Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Mkulima Duniani yamefanyika Oktoba 15, 2026, yameambatana na utoaji wa tuzo kwa wanawake watatu vinara katika kilimo, zikiwemo fedha za kununua pembejeo kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo, pamoja na uzinduzi wa kitabu cha mapishi ya viazi lishe vya rangi ya chungwa kilichoandaliwa kwa maoni kutoka sekta mbalimbali.
Shughuli hizo ni sehemu ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, yanayofanyika kitaifa jijini Tanga Oktoba 16, 2026, kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika uzalishaji wa chakula na kuhamasisha lishe bora.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...