Usimamizi shirikishi wa misitu iliyopo katika vijiji kwa jamii yenyewe inayoizunguka imesaidia katika kukuza na kuendeleza biashara ya kaboni na kuleta faida nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi wakati akichangia Majadiliano ya Kibunge kuhusu Hali ya Hewa na Uhifadhi wa Asili yaliyofanyika katika Jiji la Yerevan nchini Armenia.
Alisema kuwa Tanzania ina hekta zaidi ya milioni 2 za ardhi ya vijiji ambavyo vinajihusisha na biashara ya kaboni akitolea mfano misitu aina ya mikoko (mangrove) akieleza kuwa ina thamani kubwa zaidi.
“Msitu wa mikoko ndio wenye thamani kubwa zaidi kwani hekta moja inaweza kuhifadhi takribani tani 1,000 za hewa ya ukaa kwa mwaka, hii imeongeza thamani ya mikoko na kuongeza hamasa zaidi kwa jamii kushiriki katika biashara ya kaboni na kujipatia kipato,” alisema Dkt. Muyungi.
Akiendelea kuchangia mada, Dkt. Muyungi alizungumzia pia namna kilimo cha mwani katika pwani ya Bahari ya Hindi kinavyowainua kiuchumi wanawake akisema kuwa ni mojawapo ya mafaniko ya nchi.
Kwa upande mwingine, alisema kuwa Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, agenda ya nishati safi ya kupikia ni mojawapo ya nyenzo za kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Dkt. Muyungi alisema misitu iliyopo nchini inaweza kupotea endapo ukataji wa miti utaendelea hivyo matumizi ya nishati safi ya kupikia itasaidia kuhifadhi bioanuwai na kupunguza ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Dkt. Muyungi alisema misitu iliyopo nchini ipo hatarini kupotea endapo ukataji wa miti utaendelea hivyo agenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia itasaidia kuhifadhi bioanuwai na kupunguza ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
“Kwa hatua hiyo sisi kama Tanzania tumeshaivuka lengo la asilimia 30 ifikapo mwaka 2030, kati ya hekta milioni 48.1 za ardhi ya Tanzania tumeshahifadhi zaidi ya asilimia 33, hiyo ni kupitia hifadhi za taifa, mapori ya akiba, eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, pamoja na maeneo mengi ya vijiji ambayo yameshahifadhiwa.
Aidha, Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa dhamira na maono ya Tanzania kwa miaka 25 ijayo imezindua Dira ya Maendeleo 2050 ambayo inasema tunahitaji kuwa na uchumi wa Dola Trilioni 1 ifikapo mwaka 2050, matarajio ya kuishi miaka 75 na kipato cha mtu mmoja mmoja cha Dola 7,000.
Alisema hatua hiyo ina maana kubwa kwa namna Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inavyosimamia matamanio hayo pamoja na uhifadhi wa mazingira na bioanuwai hasa katika nguzo ya Ustahimilivu wa Mazingira
Kikao hicho cha majadiliano kilifanyika kando ya Mkutano wa 17 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Bioanuai (CBD COP17) kuanzia Oktoba 13 hadi 15, 2026 na kilishirikisha wabunge kutoka Armenia kwa lengo la kuleta manufaa yanayoonekana katika nyanja mbalimbali ili kudumisha uhifadhi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (wa kwanza kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali mara baada ya kuchangia Majadiliano ya Kibunge kuhusu Hali ya Hewa na Uhifadhi wa Asili yaliyofanyika katika Jiji la Yerevan nchini Armenia Oktoba 13 hadi 15, 2026.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...