Mkurugenzi wa Makampuni ya ASAS mkoani Iringa, Ahmed Salim Abri, ametoa Shilingi milioni sita kama mchango wake binafsi kwa Baraza la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Kata ya Miyomboni, Manispaa ya Iringa, ili kusaidia kulipia nusu ya deni la mkopo wa Shilingi milioni 12 walioupata kutoka Benki ya CRDB kupitia programu ya IMBEJU, hatua inayolenga kupunguza mzigo wa marejesho kwa wanawake hao na kuwawezesha kuelekeza nguvu zaidi katika kukuza shughuli zao za kiuchumi.
Akizungumza kwa niaba ya Ahmed Salim Abri, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Salvatory Ngerera, amesema mchango huo wa Shilingi milioni sita unaakisi dhamira ya dhati ya kiongozi huyo katika kusaidia makundi mbalimbali ya jamii kiuchumi na kijamii, kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuwawezesha kujikwamua kupitia fursa mbalimbali za maendeleo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Kata ya Miyomboni, Anna Mapembe, amemshukuru Mkurugenzi wa Makampuni ya ASAS, Ahmed Salim Abri, kwa mchango huo wa Shilingi milioni sita, akieleza kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kulipia nusu ya deni la mkopo wa Shilingi milioni 12 walioupata kutoka Benki ya CRDB kupitia programu ya IMBEJU, hivyo kupunguza mzigo wa marejesho kwa wanakikundi na kuwawezesha kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
Akizungumza kama mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhiwa hundi ya mkopo wa Benki ya CRDB kwa UWT, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Joseph Lyata, amesema chama hicho kimeendelea kujenga imani kwa wananchi kupitia usimamizi wa shughuli za maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali. Aidha, amezipongeza jumuiya za CCM kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi inayochochea maendeleo ya wanachama na kuimarisha uaminifu wao mbele ya taasisi za kifedha.
Kwa upande wake, Afisa Mikopo na Uwezeshaji wa Benki ya CRDB, Tawi la Mkwawa, Victoris Marandu, amesema benki hiyo imeendelea kukiwezesha kikundi cha UWT Kata ya Miyomboni kupitia mikopo ya programu ya IMBEJU, ambapo mkopo huo ni awamu ya pili kwa kikundi hicho. Ameeleza kuwa CRDB iko tayari kuendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi mbalimbali ili kuvichochea kukuza mitaji, kupanua shughuli za kiuchumi na kuimarisha ustawi wa wanachama wake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...