UWEKEZAJI wa kihistoria uliofanywa na China katika reli ya TAZARA umetajwa kuifufua reli hiyo kwa usafirishaji wa tani milioni 2.4 za mizigo kwa mwaka, kuimarisha biashara ya Tanzania, Zambia na DRC, huku Bandari ya Dar es Salaam ikitarajiwa kunufaika zaidi.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ufufuati ya TAZARA, Zhang Zhenhai, alisema wa Ufufuaji wa Reli ya TAZARA ni mpango mkubwa zaidi wa ukarabati na uboreshaji wa reli hiyo tangu ilipokabidhiwa na kuanza kutoa huduma mwaka 1976.

Alisema mradi huo unahusisha mtandao wa reli wenye urefu wa kilomita 1,860.543 unaopita katika nchi za Tanzania na Zambia, huku utekelezaji wake ukifanyika kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).

Mfumo huo unalenga kuunganisha uwezo, uzoefu na rasilimali za pande zinazohusika ili kuhakikisha reli inafufuliwa na kuendeshwa kwa misingi ya usalama, ufanisi na uendelevu wa kibiashara.

Moja ya malengo makubwa ya mradi huo ni kukabiliana na changamoto za muda mrefu ambazo zimekuwa zikiathiri ufanisi wa reli hiyo, ikiwemo uchakavu wa miundombinu, maeneo yanayolazimu treni kupunguza mwendo na vihatarishi mbalimbali vya kiusalama.

Changamoto hizo zimekuwa na athari katika uwezo wa reli kusafirisha mizigo kwa wakati, kuongeza safari na kukidhi mahitaji ya wateja wanaotegemea huduma zake.

Katika kutekeleza mradi huo, kipaumbele cha awali ni kufanya matengenezo muhimu na kuondoa vihatarishi vikubwa vya usalama ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya ujenzi.

Zhang alifafanua kuwa baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, kazi nyingine za ukarabati na uboreshaji zitaendelea katika kipindi cha uendeshaji, kwa awamu kulingana na mahitaji na mazingira yatakavyoruhusu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...