DAR ES SALAAM, 25 Novemba 2026.
KATIKA kipindi hiki cha likizo ambapo familia zinapata muda zaidi wa kuwa pamoja, Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Huawei inasogeza huduma ya intaneti ya kasi ya Airtel Fiber karibu na kaya katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na Arusha.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Airtel Fiber katika eneo la Makumbusho, Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, akiwa pamoja na Mgeni Rasmi, Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule, alisema kuwa wateja na wananchi
watapata fursa ya kufahamu zaidi huduma hiyo, kujionea uwezo wake, na kuelewa
jinsi intaneti ya uhakika inavyoweza kukidhi mahitaji ya kidijitali ya familia
za kisasa.
Airtel,
ambayo ni kinara wa huduma za intaneti ya nyumbani nchini Tanzania, inaendelea
kupanua wigo wa mtandao wake wa fiber (Fibre-to-the-Home - FTTX) ili kusogeza
huduma ya intaneti ya kasi karibu na makazi, ofisi, na maeneo ya biashara. Kwa
sasa, huduma ya Airtel FTTX inapatikana katika maeneo mbalimbali ya Dar es
Salaam, yakiwemo Mikocheni, Goba Matosa, Mbezi Beach, Kinyerezi, Makumbusho,
pamoja na maeneo ya Kigamboni, Nunge, OctoPrime, na KKKT Vijibweni, na Moshono
jijini Arusha.
Hatua
muhimu katika upanuzi huu ni kuzinduliwa rasmi kwa mtandao wa Airtel FTTX
katika eneo la Makumbusho, ambako miundombinu hiyo ina uwezo wa kufikia majengo
2,500 (Home Passes), na hivyo kutoa fursa kwa hadi kaya, ofisi, na
biashara 2,500 kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi ya Airtel Fiber
Katika
kipindi cha likizo, matumizi ya intaneti majumbani huongezeka kutokana na
watoto kuwa nyumbani na familia kutumia muda mwingi pamoja, hali inayofanya
intaneti ya uhakika kuwa muhimu kwa burudani, mawasiliano, elimu, na kazi. Ili
kukidhi mahitaji hayo, Airtel Fiber inatoa vifurushi visivyo na kikomo (Unlimited)
vyenye kasi ya hadi Mbps 100 na Mbps 200 (kuanzia TSh 70,000 na
TSh 100,000, vinavyowezesha familia
kutazama video mtandaoni, kucheza michezo ya kidijitali, kujifunza, na kufanya
kazi wakiwa nyumbani kwa ufanisi bila changamoto za video kukwama au mawasiliano
kukatika.
Akizungumzia
hatua hiyo, Charles Kamoto, Mkurugenzi Mtendaji wa
Airtel Tanzania, alisema kampuni inaendelea kuwekeza katika
teknolojia ya kisasa ili kusogeza intaneti ya uhakika karibu na wananchi na
kuwawezesha kunufaika na mabadiliko ya kidijitali.
“Tanzania
inapitia mabadiliko makubwa ya kidijitali, na kiini cha mabadiliko hayo ni
upatikanaji wa intaneti ya uhakika. Kupitia Airtel Fiber, tunasogeza teknolojia
ya kisasa karibu na wakazi wa Makumbusho, kwa kasi ya Mbps 100 na Mbps 200
kulingana na mahitaji ya mteja. Tunataka familia na biashara zinufaike na
mawasiliano ya kasi yanayorahisisha maisha, kazi na shughuli zao za kila siku,”
alisema Kamoto.
Ili
kufanya huduma hiyo ipatikane kwa urahisi zaidi, Airtel inatoa ofa ya Double Benefit Impact with Airtel Fiber, inayowawezesha wateja wapya kupata ofa ya mwezi
mmoja wa intaneti bila malipo wanapojisajili kwa mara ya kwanza na kuchagua
kifurushi chenye thamani ya kati ya Shilingi 70,000 na Shilingi 100,000.
Ofa hii inawapa wateja nafasi ya kufurahia intaneti ya kasi ya nyumbani huku
wakipata thamani zaidi ya huduma wanayolipia.
Ofa
hiyo inakuja wakati muafaka kwa familia zinazotaka kufurahia burudani pamoja,
kuwawezesha watoto kutumia rasilimali za kujifunzia mtandaoni, kuwasiliana na
ndugu na marafiki, pamoja na kuendelea na shughuli za kazi na biashara wakiwa
nyumbani katika kipindi hiki cha likizo.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mhe. Saad Mtambule, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Mgeni
Rasmi, aliipongeza Airtel Tanzania na Huawei kwa kusogeza huduma ya
intaneti ya kasi karibu na wananchi, akieleza kuwa mawasiliano ya uhakika yana
mchango muhimu katika maendeleo ya jamii na uchumi.
“Intaneti
ya kasi na ya uhakika ni muhimu kwa maendeleo ya jamii na uchumi. Kupitia
Airtel Fiber, wafanyabiashara wa Makumbusho watapata fursa ya kutangaza bidhaa
zao mtandaoni, kuwafikia wateja wengi zaidi na kuendesha biashara zao kwa
ufanisi. Ninawahimiza wananchi kutumia huduma hii na kunufaika na fursa za
uchumi wa kidijitali,” alisema Mhe. Mtambule.
Kupitia
ushirikiano wake na Huawei, Airtel inaendelea kuimarisha huduma zake za
intaneti ya nyumbani kwa kutumia teknolojia na miundombinu ya kisasa inayolenga
kuwapatia wateja intaneti ya kasi na huduma bora zaidi.
Franklin Huang, Makamu wa Rais wa Huawei Tanzania, alisema ushirikiano huo unaonesha umuhimu wa
kuunganisha utaalamu wa kiteknolojia na miundombinu ya mawasiliano ili kusogeza
intaneti ya kasi karibu na kaya na biashara nyingi zaidi.
“Intaneti
imekuwa muhimu katika kujifunza, kufanya kazi, kuwasiliana na kukuza biashara.
Kupitia ushirikiano wetu na Airtel Tanzania, tunatoa teknolojia inayosaidia
kupanua miundombinu ya nyuzi za mawasiliano na kusogeza intaneti ya kasi karibu
na kaya na biashara nyingi zaidi. Tunajivunia kushirikiana na Airtel katika
kujenga Tanzania iliyounganishwa zaidi,” alisema Bw. Huang.
Kadri
Watanzania wanavyozidi kutumia teknolojia katika shughuli zao za kila siku,
Airtel Tanzania inaendelea kujizatiti kupanua upatikanaji wa intaneti ya
nyumbani na kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za elimu, biashara,
mawasiliano na burudani zinazopatikana kupitia huduma za kidijitali.
Likizo
hii, wasogeze familia na marafiki karibu zaidi kwa Airtel Fiber. Furahia kasi.
Furahia mawasiliano. Furahia mengi zaidi na Airtel Fiber.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...