Timu maarufu ya mbio za magari nchini, ASAS Rally Team, kupitia mpango wa kijamii wa ASAS Maziwa Mashuleni, imeandaa zoezi la kugawa maziwa kwa wanafunzi katika shule 10 za Jiji la Arusha, ikiwa ni sehemu ya juhudi za ASAS Group za kuunga mkono afya, lishe na ustawi wa watoto nchini Tanzania.

Katika zoezi hilo, jumla ya pakiti 6,000 za maziwa zinatarajiwa kugawiwa kwa wanafunzi, kwa lengo la kuhamasisha umuhimu wa lishe bora katika ukuaji, afya na maendeleo ya elimu.

Hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya ASAS Group ya kuhakikisha kuwa shughuli zake za kibiashara na michezo zinakwenda sambamba na utekelezaji wa miradi yenye manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...