- Wateja watapata fursa ya kujishindia zawadi za kila wiki na kila mwezi, pamoja na zawadi kuu ya shilingi milioni 15 katika droo ya mwisho wa kampeni.
Benki ya Exim Tanzania imezindua kampeni ya miezi mitatu ya ‘Maliza Kirahisi Kidigitali-Kamata Kitita’, inayolenga kuwahamasisha wateja wake kutumia huduma za kibenki za kidijitali katika miamala yao ya kila siku, huku wakipata fursa ya kujishindia zawadi za fedha taslimu.
Kampeni hiyo, itakayoendeshwa kuanzia Novemba 2026 hadi Februari 2027, ni sehemu ya juhudi za Benki ya Exim Tanzania za kuendelea kuimarisha nafasi yake katika utoaji wa huduma za kifedha zinazotumia teknolojia na ubunifu. Kwa uzoefu wake katika sekta ya huduma za kifedha, benki imeendelea kuwekeza katika mifumo ya kisasa na kupanua njia zake za huduma za kidijitali, ikiwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi, haraka na kwa uhakika.
Huduma hizi zinapatikana kupitia njia mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na benki, zikiwemo Exim Pay na USSD *150*11#, Internet Banking, Exim WhatsApp Banking, Exim Wakala na Exim Mastercard. Kupitia njia hizi, wateja wanaweza kutuma fedha, kulipia bili, kununua umeme, kufanya manunuzi na kusimamia akaunti zao.
Upatikanaji wa huduma kupitia njia hizi mbalimbali unawapa wateja uhuru wa kuchagua huduma inayowafaa kulingana na mahitaji na mazingira yao, huku ukiwawezesha kufanya miamala kwa urahisi na kuokoa muda bila kulazimika kutembelea tawi la benki kwa kila huduma.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala ya kidijitali wa Benki ya Exim Tanzania, Silas Matoi, alisema kampeni hiyo imeandaliwa kuwapa wateja fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali, ikiwemo zawadi kuu ya shilingi milioni 15.
“Tunataka wateja wetu waweze kufanya miamala yao ya kila siku kwa urahisi kupitia njia mbalimbali za kidijitali. Katika kampeni hii, wateja 30 watajishindia shilingi 50,000 kila mmoja katika droo za kila wiki, huku wateja 10 wakijishindia shilingi 500,000 kila mmoja katika droo za kila mwezi”.
“Aidha, katika droo kuu ya mwisho wa kampeni, washindi watatu watajishindia zawadi za shilingi milioni 5, milioni 10 na milioni 15, kulingana na nafasi zao. Tunawahamasisha wateja kutumia huduma zetu za kidijitali na kutimiza vigezo vya kampeni ili waweze kujishindia zawadi hizo,” alisema Matoi.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Kauthar D'souza, alisema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja kutumia huduma za kidijitali za Exim katika shughuli zao za kila siku huku wakipata fursa ya kujishindia zawadi.
“Tunawahamasisha wateja wetu kutumia huduma za Exim za kidijitali wanapofanya miamala yao ya kila siku. Pamoja na urahisi wanaoupata, wanapata pia fursa ya kuwania zawadi kupitia kampeni hii. Tunawakaribisha wateja wote kushiriki kwa kutumia huduma zetu za kidijitali na kutimiza vigezo vilivyowekwa. Ujumbe wetu ni rahisi: Maliza Kirahisi Kidigitali-Kamata Kitita!” alisema D'souza.
Kwa upande wake, Afisa Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha, Pendo Albert Mfuru, alisema droo za kampeni hiyo zitaendeshwa kwa mfumo wa kielektroniki unaochagua washindi kwa nasibu, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Alisisitiza kuwa usimamizi huo unalenga kuhakikisha mchakato wa upatikanaji wa washindi unafanyika kwa haki na uwazi.
“Tunathamini juhudi za kampuni zinazotoa promosheni zenye zawadi kwa wateja wao. Katika kampeni hii, tutasimamia mchakato wa droo ili kuhakikisha unafanyika kwa haki na uwazi, huku washiriki wanaotimiza vigezo na masharti wakipata nafasi ya kuwania zawadi,” alisema Mfuru.
Kampeni ya ‘Maliza Kirahisi Kidigitali-Kamata Kitita’ ni sehemu ya juhudi za Benki ya Exim Tanzania za kuendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia na ubunifu katika utoaji wa huduma za kifedha. Kupitia kampeni hii, benki inalenga kuwahamasisha wateja kutumia njia zake mbalimbali za kidijitali katika miamala yao ya kila siku, wakinufaika na urahisi na uhakika wa huduma hizo huku wakipata fursa ya kujishindia Zawadi.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...