-Kampeni inaendeleza mafanikio ya Mtandao wa Viwango kwa kuwazawadia wateja waliochagua Yas

Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania imezindua ‘Magifti ya Viwango’, Kampeni ya miezi mitatu katika msimu huu wa sikukuu inayowapa wateja wake kote nchini fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo gari jipya lenye thamani ya shilingi milioni 100, shilingi milioni moja kila siku, simu janja mpya aina ya iPhone 18 kila wiki na shilingi milioni 10 kila mwezi.

Kampeni hiyo inalenga kusherehekea Mwaka wa Viwango, katika kipindi ambacho Yas Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kuimarisha mtandao wake. Mafanikio hayo yametokana na uwekezaji katika kupanua wigo wa mtandao, kuongeza uwezo wake na kuimarisha uthabiti wake.

Mpaka sasa, Yas inajivunia kuwa na mtandao wenye kasi zaidi na unaofika katika maeneo mengi zaidi nchini. Mtandao huo una zaidi ya minara 4,900 huku teknolojia yake ya 5G ikiendelea kupanuka sambamba na teknolojia mpya kama VoLTE. Hatua hizo zinawawezesha watu binafsi, wafanyabiashara na taasisi kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa Mkuu wa Teknolojia na Ufundi - Yas Tanzania, Bw. Emmanuel Mallya, alisema,

“Uwekezaji wetu wa zaidi ya shilingi trilioni 1.2 kwenye mtandao unadhihirisha dhamira yetu ya kuwapatia Watanzania huduma bora za mawasiliano. Tumeendelea kupanua wigo wa mtandao wetu, kuongeza uwezo wake na kuimarisha uthabiti wake ili kuwawezesha wateja kufanya mambo mengi zaidi kupitia teknolojia. Iwe ni kupiga simu, kutazama maudhui mtandaoni, kujifunza, kufanya kazi au kuendesha biashara, tunataka kuhakikisha mtandao wetu unarahisisha shughuli zao za kila siku,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara wa Yas Tanzania, Bw. Norman Kiondo, alisema mtandao imara na wa kisasa una mchango mkubwa katika kuharakisha mageuzi ya kidijitali. Aliongeza kuwa mtandao wa aina hiyo pia unaongeza ushindani wa biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.

“Tunaposherehekea Mwaka wa Viwango, biashara nyingi zaidi nchini zinakumbatia teknolojia ya kidijitali ili kukua na kutengeneza fursa mpya. Lengo letu si tu kutoa mtandao unaoendesha uchumi wa kidijitali, bali pia kutoa suluhisho za kidijitali zitakazosaidia biashara kujiendesha kwa ufanisi na kukua,” alisema Bw. Kiondo.

Kampuni hiyo imesema kuwa uwekezaji wake unaendelea kufungua fursa kote nchini. Hata hivyo, mafanikio ya Mwaka wa Viwango yasingewezekana bila wateja walioendelea kuiamini na kutumia huduma zake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Yas Tanzania, Bi. Mwangaza Matotola, alisema kampeni hiyo inaendeleza utamaduni wa kampuni hiyo wa kila mwaka wa kuwathamini na kuwazawadia wateja wake zaidi ya milioni 34.

“Magifti ya Viwango ni njia yetu ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuamini na kuwa sehemu ya safari yetu ya ukuaji. Wateja wetu ndio kiini cha Mwaka wa Viwango, na kupitia kampeni hii tunasherehekea pamoja nao. Tunataka wauamalize mwaka kwa furaha na kuuanza mwaka mpya kwa kishindo na matumaini makubwa zaidi,” alisema.

Aliongeza kuwa zawadi za kampeni hiyo zimechaguliwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kila siku ya wateja. Zawadi hizo zinaweza kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kukuza biashara zao na familia kukabiliana na gharama mbalimbali, hususan mwanzoni mwa mwaka.

“Tunatambua kuwa zawadi hizi zina maana tofauti kwa watu tofauti. Kwa mfanyabiashara mdogo, fedha taslimu zinaweza kuwa mtaji wa kukuza biashara yake. Kwa familia, zinaweza kusaidia kumudu gharama za kurudi shule na mahitaji mengine ya nyumbani. Na kwa mshindi wa gari, ni fursa ya kuboresha maisha yake,” alisema Bi. Matotola.

Kupitia kampeni hiyo, wateja watapata nafasi ya kujishindia shilingi milioni moja kila siku, simu janja aina ya iPhone 18 kila wiki na shilingi milioni 10 kila mwezi. Aidha, kutakuwa na zawadi maalum za sikukuu za fedha taslimu za shilingi milioni 10 na shilingi milioni 5. Zawadi kuu itakuwa gari jipya lenye thamani ya shilingi milioni 100.

Akielezea namna ya kushiriki, Bi. Matotola alisema kila kifurushi kitakachonunuliwa kupitia Yas App, kwa kubonyeza *147*00# au kupitia Yas Rusha kitampa mteja nafasi ya kuingia kwenye droo. Wateja pia watapata nafasi za ziada kwa kulipia bili za huduma ya intaneti ya Fiber na kufanya marejesho ya mikopo ya ununuzi wa vifaa. Kupakua na kujisajili kwenye Yas App pia kutawapa nafasi za ziada.

“Tunataka wateja wetu waendelee kufurahia huduma wanazotumia kila siku huku wakipata fursa ya kujishindia zawadi kabambe. Kadiri mteja atakavyofanya manunuzi na malipo mengi zaidi, ndivyo atakavyoongeza nafasi yake ya kushinda,” alisema.

Kwa upande wake, Japhet Mwaikenda, mteja wa Yas anayeishi jijini Dar es Salaam, alishiriki katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Alisema zawadi za fedha taslimu zitakuwa msaada mkubwa kwa familia katika kukabiliana na gharama za mwanzoni mwa mwaka.

“Mwezi Januari huwa na majukumu mengi ya kifedha, yakiwemo kulipa ada za shule na kugharamia mahitaji mengine ya familia. Hivyo, kujishindia shilingi milioni moja kutakuwa msaada mkubwa kwa familia yangu. Kwa kuwa tayari ninanunua vifurushi kwa ajili ya kupiga simu na kutumia intaneti, kupata nafasi ya kushinda kupitia manunuzi hayo ni motisha ya ziada kwangu,” alisema.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...