Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Morogoro
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mwigulu Nchemba amempongeza Joyce Shebe kwa kushinda uchaguzi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa jukwaa hilo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Novemba 26,2026 mjini Morogoro umehusisha wapiga kura 141 ambao ni wanachama wa jukwaa hilo ambapo Shebe ameshinda kwa kura 88 sawa na asilimia 62.4 dhidi ya kura 53 sawa na asilimia 37 alizopata Salome Kitomari.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Waziri Mkuu Dk.Mwigulu Nchemba amempongeza Makamu Mwenyekiti Joyce Shebe kwa ushindi alioupata.
“Hongera Makamu Mwenyekiti kwa kuchaguliwa katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti .Wakati unatambulisha waliopo katika mkutano huu nimejiridhisha kuhusu uwezo na nimejua umeshindaje uchaguzi.
“Unao uwezo mkubwa na mimi katika timu ninayoipenda huko nyuma tuliwahi kuwa na Kocha Jack Chamangwana ambaye alikuwa akisema mchezaji mzuri utamjua tu wala hauitaji muda mrefu.Makamu Mwenyekiti katika huu muda mfupi uliozungumza umeonesha uwezo mkubwa.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile amesema kuwa ushindi wa Makamu Mwenyekiti Joyce Shebe ni ushindi wa TEF na baada ya uchaguzi jukwaa hilo limebakia kuwa moja huku akieleza uchaguzi ulikuwa wa demekrasia na umetoa somo la kufanya uchaguzi.”Mshindi wa TEF amepatikana katika boksi la kura.”


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...