Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini mkoani Pwani Silvester Koka, ameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maji na barabara katika Manispaa ya Kibaha, akieleza kuwa baadhi ya miradi hiyo imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Amesema miongoni mwa miradi inayotia wasiwasi ni ujenzi wa tenki la maji la Pangani, ambao licha ya kusainiwa kwa mkataba takribani miaka mitatu iliyopita, umefikia asilimia 13 pekee ya utekelezaji.
Akizungumza leo Novemba 18,2026 mbele ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, Koka amesema mradi huo ni muhimu kwa wakazi wa Kata ya Pangani na maeneo jirani ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Ametaja maeneo yanayohitaji huduma hiyo kuwa ni Mpapa, Pangani, Mdeja, Majimoto na Lulanzi, akisema wananchi wake wameendelea kuhangaika kutafuta maji licha ya mradi huo kuanza kutekelezwa
Amesema hali hiyo inahitaji uingiliaji wa Serikali ili mkandarasi aharakishe kazi na kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji huo badala ya kuendelea kusubiri huduma muhimu.
Katika hatua nyingine, mbunge huyo ameiomba Serikali kuongeza kasi ya upanuzi wa barabara ya Morogoro, akieleza kuwa eneo la Kibaha limekuwa likikabiliwa na msongamano mkubwa wa magari kutokana na shughuli za kiuchumi na usafiri kuelekea mikoa ya Magharibi.
Ameongeza magari mengi yanayoingia na kutoka Dar es Salaam yanapita katika eneo hilo, huku sehemu kubwa ya msongamano ikijitokeza kati ya Kibaha na Chalinze, hali inayopoteza muda na kuongeza gharama za usafirishaji.
Koka amesema barabara hiyo ni miongoni mwa miundombinu muhimu zaidi kiuchumi nchini, hivyo Serikali inapaswa kuipa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya upanuzi.
Pia ameeleza kusuasua kwa mradi wa barabara ya Chang’ombe–Mapinga yenye urefu wa takribani kilomita 25, akisema hadi sasa ni kilomita 10 pekee zilizojengwa.
Ameongeza kuchelewa kukamilika kwa miradi ya aina hiyo kunachelewesha manufaa yaliyokusudiwa na kuongeza gharama za utekelezaji, hivyo akaiomba Serikali kuingilia kati ili kuhakikisha mradi huo unakamilika
Kuhusu usafiri wa umma, Koka amesema wananchi wa Kibaha Mjini bado hawajanufaika na huduma ya mwendokasi licha ya miundombinu ya barabara kujengwa na kuwepo kwa mazingira ya kuanza kwa huduma hiyo.
Ameiomba Serikali kuharakisha maandalizi na kuweka utaratibu utakaowezesha wananchi kuanza kutumia usafiri huo, akisema utasaidia kupunguza adha ya usafiri kati ya Kibaha na Dar es Salaam.
“Barabara hizo zina umuhimu mkubwa katika kufungua fursa za biashara, uwekezaji na usafirishaji wa bidhaa, hasa kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.”
Aidha, ameelezachangamoto ya daraja la Lunguki linalopita Mto Mpiji na kuunganisha Kata ya Pangani na maeneo ya Mkamba, Maringota pamoja na Wilaya ya Mkuranga.
Amefafanua daraja hilo limekuwa likikumbwa na changamoto ya mabadiliko ya mkondo wa mto, hali inayosababisha wananchi kushindwa kuvuka kwa urahisi, huku watoto wakipata wakati mgumu kufika shuleni na wafugaji wakikabiliwa na changamoto ya kuvusha mifugo.
Ameiomba Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mkuranga kutafuta suluhisho la kudumu la ujenzi wa daraja hilo ili kurahisisha mawasiliano na shughuli za kiuchumi.
Pamoja na changamoto hizo, Koka ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika maendeleo ya Manispaa ya Kibaha, akisema hatua mbalimbali zimeongeza kasi ya utoaji wa huduma za kijamii.
Pia amesema Halmashauri imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2026/27 ilikuwa imekusanya takribani Shilingi milioni 18, sawa na asilimia 55.5 ya makadirio ya kipindi hicho.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2026/27, takribani Shilingi milioni 600 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii.
Katika sekta ya elimu, amesema Serikali imejenga shule mpya za msingi 12 na sekondari 10, huku ujenzi wa madarasa na maabara ukiendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Ameongeza hatua hizo zimechangia kuongezeka kwa ufaulu, kiasi cha shule za sekondari za kata kuanza kushindana na shule binafsi katika matokeo ya mitihani.
Kuhusu afya, amesema Halmashauri imeendelea kuboresha huduma kwa kujenga vituo vya afya na zahanati, huku upatikanaji wa dawa ukiongezeka ikilinganishwa na hali ya awali.
Serikali pia imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya barabara, maji na umeme, akitaja utekelezaji wa miradi ya maji yenye thamani ya Shilingi milioni 700.5 na ujenzi wa miundombinu mingine ya kusogeza huduma karibu na wananchi.
Koka alihitimisha kwa kuiomba Serikali kuyafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa, akisema kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua fursa za uwekezaji, kuongeza shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wakazi wa Kibaha Mjini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...