Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner, leo Novemba 18, 2026, jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao, wamefanya tathmini ya ushirikiano baina ya taasisi zao kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na maendeleo baina ya baina ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amemshukuru Bw. Schreiner kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na UNFPA, hususan katika masuala ya idadi ya watu na mipango ya maendeleo.

Dkt. Kida amesisitiza umuhimu wa kuzingatia mwenendo wa idadi ya watu, uwekezaji kwa vijana na maendeleo ya rasilimali watu katika utekelezaji wa Dira 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.
Aidha, amesisitiza kuwekeza kwa vijana, kuimarisha rasilimali watu na kukabiliana na changamoto za umaskini, mimba za utotoni na ukatili wa kijinsia ili Taifa liweze kunufaika na fursa za idadi kubwa ya vijana.

Aidha, viongozi hao wamekubaliana kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu na kuandaa programu mpya ya ushirikiano inayoakisi vipaumbele vya Dira 2050.

Kwa upande wake, Bw. Schreiner amethibitisha dhamira ya UNFPA kuendeleza ushirikiano huo, ikiwemo kutoa msaada wa kitaalamu katika uchambuzi wa takwimu na mwenendo wa idadi ya watu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...