Vodacom Tanzania Plc imetoa ripoti yake ya nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2027 ikionesha ongezeko la mapato yatokanayo na huduma kwa asilimia 20.8 hadi Sh trilioni 1.067 huku faida baada ya kodi ikipanda kwa asilimia 182.7 hadi Sh bilioni 117.8.

Ukuaji huo katika kipindi cha miezi sita kilichoishia Septemba 30, 2026, umechangiwa na huduma za M-Pesa na data za simu, ambazo mapato yake yameongezeka kwa asilimia 26.2 na 24.6 mtawalia. Idadi ya wateja wa kampuni hiyo imeongezeka kwa asilimia 17 na kufikia milioni 29.2, huku watumiaji wa huduma za data na M-Pesa wakiongezeka kwa asilimia 13.9 na 14.1 mtawalia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Philip Besiimire, alisema matokeo hayo yanaakisi kuongezeka kwa wateja na matumizi ya huduma za kampuni, pamoja na uwekezaji unaoendelea katika mtandao na teknolojia. 

Aidha katika kipindi hicho, kampuni iliwekeza Sh bilioni 246 kuimarisha miundombinu na kupanua upatikanaji wa huduma za kidijitali na kifedha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Hilda Bujiku, alisema matokeo hayo yanaonesha uimara wa kifedha wa kampuni, unaotokana na ukuaji wa mapato na faida, pamoja na kuongezeka kwa fedha zinazotokana na shughuli za biashara. Hali hiyo inaiwezesha kampuni kuendelea kugharamia uwekezaji wake katika miundombinu ya mtandao na teknolojia.

Soma zaidi: https://vodacom.co.tz/assets/uploads/Vodacom_Tanzania_interim_condensed_consolidated_financial_results_2026_4286e52015.pdf?_gl=1*6qlh5p*_gcl_au*MTA3NzYyMTYwMS4xNzkwODU3NjY1



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...